Mahakama nchini Rwanda imekataa ombi la kumwachia kwa dhamana mshitakiwa wa mauaji ya kimbari, Jean Uwinkindi huku Shirika moja nchini Ufaransa likitangaza kuandaa mashitaka mpya dhidi ya wanyarwanda wanatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari wanaoishi nchini humo.
RWANDA
Uwinkindi anyimwa dhamana: Mahakama mjini Kigali, Jumatano ilikataa ombi la kumwachia kwa dhamana mshitakiwa wa mauaji ya kimbari, Jean Uwinkindi kutokana na kilichoelezwa na mahakama hiyo kuwa ‘’uzito wa mashitaka anayokabiliwa nayo na wasiwasi kwamba huenda atatoroka.’’Mchungaji Uwinkindi anashitakiwa kwa mauaji ya kimbari na kuteketeza kizazi.Inadaiwa kwamba mchungaji huyo alihamasisha na kuongoza mauaji dhidi ya Watutsi katika parokia yake ya Kayenzi wakati wa mauaji hayo mwaka 1994. Wakili kiongozi wa mshitakiwa huyo, Gatera Gashabana alisema kuwa atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.Mchungaji Uwinkindi alitiwa mbaroni Juni 30, 2010 nchini Uganda na kuhamishiwa makao makuu ya ICTR, mjini Arusha, Tanzania, siku mbili baadaye.Aprili 19, 2012 akawa mshitakiwa wa kwanza wa ICTR, kesi yake kuhamishiwa nchini Rwanda kwenda kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya nchi hiyo. Alikana tuhuma zote dhidi yake.
UFARANSA
Walalamikia Ufaransa kutowashitaki watuhumiwa wa mauaji ya kimbari: Shirika moja nchini Ufaransa Jumanne wiki hii limesema linaandaa malalamiko mapya dhidi ya Wanyarwanda wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kimbari wanaoishi nchini humo. Shirika hilo, Collective de parties cevile poa le Rwanda limesema kwamba hatua hiyo inafuatia ziara ya waliyofanya nchini Rwanda hivi karibuni.Shirika hilo limefafanua kwamba limeshafungua malalamiko zaidi ya 10 mbele ya mahakama nchini Ufaransa lakini hakuna hata kesi moja iliyoshuhgulikiwa.Rais wa Shirika hilo, Alain Gauthie amesema kwamba wanashindwa kuivumilia hali hiyo lakini hawajakata tama. Aliisifu ziara iliyofanywa nchini Rwanda na kutoa wito kwamba haina budi kufuatiwa na kushitakiwa kwa wahusika. Rais huyo alieleza pia kwamba kesi mbili zilizopelekwa nchini Rwanda inayowahusi afisa mmoja na mchungaji toka Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) pia zisikilizwe.
WIKI IJAYO
ICC
Kesi ya Bemba kuendelea kusikilizwa Jumatatu: Kesi inayomkabili kiongozi wa zamani wa kundi la waasi la Jamhuri ya Kideokrasi ya Congo (MLC) Jean Pierre Bemba itaendelea kusikiliza Jumatatu ijayo, Septemba 3, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kwa kuendelea kupata ushahidi kutoka kwa mashahidi wa utetezi. Bemba anakabiliwa na mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita unaodaiwa kufanywa kati ya mwaka 2002 na 2003 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia