Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja
JESHI la Polisi nchini limeunda tume itakayochunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, Marehemu Daud Mwangosi kilichotokea mjini Iringa wakati Jeshi la Polisi likipambana na wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ufunguzi wa tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja amesema kuwa Uchunguzi huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) "Jeshi la Polisi limeunda tume itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pamoja Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo" alisema Chagonja.
Marehemu Mwangosi amefariki dunia jana wakati baada ya kulipukiwa na kitu kinachachodaiwa kuwa ni bomu wakati chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) kikifungua tawi la chama vchake katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.
"Kwa sasa tayari Ispekta Generali wa Polisi (IGP), Said Mwema yupo mjini Iringa pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba pamoja na timu yake nzima kuanza rasmi kwa uchunguzi wa tukio hilo. Alisema Kamishna Chagonja".
"Kwa sasa tayari Ispekta Generali wa Polisi (IGP), Said Mwema yupo mjini Iringa pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba pamoja na timu yake nzima kuanza rasmi kwa uchunguzi wa tukio hilo. Alisema Kamishna Chagonja".
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia