TCRA KUONDOA VOCHA ZA KUKWANGUA KUANZIA JANUARI 2027

 

Na Mwandishi wetu.

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza mpango wa kuondoa matumizi ya kadi za kukwangua za muda wa maongezi ili kuongeza matumizi ya njia za kidijitali.

TCRA imesema mpango huo utachangia kupunguza uzalishaji, usambazaji na utupaji wa kadi za kukwangua za muda wa maongezi pamoja na athari zake kwa mazingira, huku ukiunga mkono maendeleo ya sekta ya mawasiliano yenye ufanisi na inayotumia teknolojia za kidijitali.

Aidha, imeongeza kuwa zoezi la majaribio ya kusitisha matumizi ya kadi hizo litaanza Januari 1, 2027 likitanguliwa na shughuli za uhamasishaji kwa umma zilizoanza Oktoba 1, 2026.


TCRA imesema zoezi la majaribio litahusisha Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma (Jiji la Dodoma, Chamwino, Kondoa Mjini na Kongwa), Arusha (Jiji la Arusha, Wilaya ya Arusha, Meru na Karatu), Mwanza (Nyamagana, Ilemela na Misungwi) na Mbeya (Jiji la Mbeya, Wilaya ya Mbeya na Mbarali).




About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia