WAANDISHI WA KIMATAIFA WAKOSHWA NA UZURI WA NGORONGORO
Waandishi nguli wa habari za michezo
na burudani kutoka sehemu mbalimbali duniani, walioko nchini Tanzania
kwa ziara ya kiutalii na kufuatilia maandalizi ya AFCON 2027, Oktoba 5,
2026 wamefika katika Hifadhi ya Ngorongoro na kushuhudia utajiri wa
vivutio vya utalii nchini.
Katika ziara hiyo, waandishi hao
wamejionea wanyamapori mbalimbali wakiwemo simba, faru, twiga na
wengine, huku wakipata fursa ya kutembelea pia Makumbusho ya Binadamu wa
Kale na kujifunza historia ya mwanadamu.
Waandishi hao wamesema
ziara hiyo imewapa picha halisi ya Tanzania, wakisisitiza kuwa wageni
watakaokuja nchini kwa ajili ya AFCON 2027 hawatapata fursa ya kufurahia
mpira pekee, bali pia watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali
na kujionea uzuri, historia na utamaduni wa Tanzania.
“Hii ndiyo
Tanzania! Ukija kwa AFCON 2027, hutafurahia mpira tu—utapata pia nafasi
ya kugundua maajabu ya Tanzania kama Ngorongoro.”.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia