WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AWASILI UINGEREZA

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Oktoba 7, 2026, amewasili nchini Uingereza, ambako anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Jukwaa la Uwekezaji la Tanzania nchini humo.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu ataongoza ujumbe wa Tanzania katika mikutano na wadau, wawekezaji pamoja na viongozi wa kampuni mbalimbali zinazofanya shughuli katika sekta za madini, benki, teknolojia, usafirishaji na miundombinu.

Mikutano hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji, pamoja na kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana nchini Tanzania kwa wawekezaji kutoka Uingereza na maeneo mengine.






About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia