PROF. GEORDAVIE: AMANI SI UKOSEFU WA MIGOGORO, BALI NI UWEPO WA HAKI NA UTU

 



Na Mwandishi Wetu, Doha – Qatar

NAIBU Mwenyekiti wa United Nations Peace Ambassadors Foundation (UN-PAF), Mhe. Nabii Mkuu Prof. GeorDavie, amesema amani ya kweli haipimwi kwa ukosefu wa migogoro pekee, bali kwa uwepo wa haki, utu, fursa, kuheshimiana na uwajibikaji wa pamoja.

Prof. GeorDavie aliyasema hayo alipokuwa akihutubia Mkutano wa UN-PAF Doha International Peace & Diplomatic Forum 2026, uliofanyika jijini Doha, Qatar, akizungumzia umuhimu wa kuimarisha ujenzi wa amani katika Ukanda wa Ghuba.

Alisema ujenzi wa amani ya kudumu lazima uanze na mazungumzo na kuundwa kwa majukwaa imara yatakayowawezesha serikali, wanadiplomasia, mashirika ya kiraia, viongozi wa dini, vijana na jamii kuwasiliana kwa uwazi, kwa heshima na kwa njia yenye kujenga.

"Ghuba ni eneo lenye umuhimu wa kimkakati duniani, likiunganisha mataifa, tamaduni, uchumi na ustaarabu mbalimbali Kuendelea kwa utulivu wake si jukumu la kikanda pekee, bali ni maslahi ya dunia nzima," alisema Prof. GeorDavie.


Alisisitiza haja ya kuimarisha diplomasia ya kuzuia migogoro, akibainisha kuwa ni bora zaidi kutatua tofauti kupitia mazungumzo na maelewano kabla hazijageuka kuwa migogoro mikubwa.

"Nchi za Ghuba zimeonesha kwamba diplomasia inaweza kuleta matokeo ya kushangaza tunapaswa kujenga juu ya utamaduni huu kwa kuendeleza mazungumzo ya kikanda, ushirikiano wa kibinadamu, uendelevu wa mazingira na utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani," aliongeza.


Alimalizia kwa kusisitiza kuwa, "Amani si tu kutokuwepo kwa migogoro amani ni uwepo wa haki, utu, fursa, kuheshimiana na uwajibikaji wa pamoja."


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia