DC ARUSHA ATAPELIWA MILINI 10 NA WEZI WA MTANDAO

 mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu akiwa ofisini kwake anaongea na waaandishi jinsi alivyotapelewa shilingi milioni kumi na wezi wa mitandao
Mkuu wa wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu akiwa anaonyesha ujumbe mfupia wa maneno ambao matapeli hao walikuwa wanatuma kwa watu

Na Woinde Shizza ,Arusha.



Mkuu wa Wilaya ya Arusha Fadhili Nkulu ameibiwa kiasi cha shilingi milioni 10 na wezi wa mtandao ambao waliteka mawasiliano yake ya simu za mkononi kwa muda wa saa 3 na kutumia namba hizo kuomba fedha kwa watu wa karibu na kiongozi huyo.



Akizungumza na waandishi wa Habari Ofisini kwake ,Nkulu amesema kuwa jana majira ya saa 10:00 alasiri simu zake zilikua hazipatikani hewani mpaka majira ya saa 3:00  usiku ndipo aliposhtuka na kuanza kufuatilia na kugundua kuwa mawasiliano yake yalitekwa kwa muda.



Mkuu huyo wa Wilaya amelaani  vitendo vya wizi wa mtandao vinavyofanywa na watu wenye nia ovu huku akiwataka wananchi na wamiliki wa makampuni ya simu kuwa makini juu ya wizi huo wa kimtandao ambao umeshamiri miaka ya hivi karibuni.



Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa Yoitham Ndembeka ambaye alitumiwa ujumbe wa kumtaka atume fedha kupitia namba ya mkuu huyo wa wilaya  amesema kuwa baada ya kusumbuliwa na matapeli hao ambao hawakutaka kupokea simu aliamua kuachana nao huku akitafuta namna ya kuonana ana kwa ana na Mkuu huyo wa Wilaya.



Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel kanda ya Kaskazini alipotafutwa kujibu madai hayo simu yake haikupatikana hewani.



Wizi wa mitandao umeshamiri na kushika kasi hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia imekua kwa kiasi kikubwa ,hivyo makapuni ya simu,mamlaka za kusimamia teknolojia ya mawasiliano TCRA pamoja na polisi wanapaswa kuchukua hatua kupambana na uhalifu huo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post