Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona wa tatu kulia akiwa anaonyeshwa moja ya madini ya vifo yalioletwa katika maonyesho ya wafanyabiashara wa ndani wa madini hayo yaliyofanyika ndani ya mji mdogo wa mirerani mkoani Manyara
Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer akiwa anaonyesha jiwe la Tanzanite ambalo lipo tayari kuuzwa
Idha benki ya NMB ilimefungua rasmi tawi katika mji huu ndogo wa mererani hapa meneja wa mji mdogo wa benki hiyo akiwa anamueleza mkuu wa wialaya pamoja na wananchi waliouthuria semina hiyo huduma ambazo wanazitoa benki hiyo ndani ya mji mdogo wa mirerani
Mkuu wa wilaya akiwa anakata utepe hii ikiwa ni ishara ya kufunguliwa rasmi kwa maonyesho hayo ya vito na madini
Wafanya biashara wakubwa ambao ni wa pili kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya Jacaranda Holding DR,Antony Haj Frisby akiwa na mwenzake wanachagua madini ya vito kwa ajili ya kuyanunua ambapo alisema kuwa maonyesho haya ni mazuri sana ila aliomba wachimbaji wadogo wajitokeze kwawingi kuleta bidhaa zao.
habari picha na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog,Mererani
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Mahmoud Kambona amewaagiza
wote waliovamia na kujikatia viwanja au kujenga kwenye eneo huru la
usafirishaji bidhaa nje (EPZA) waondoke na kubomoa kabla hawajaondolewa kwa
nguvu.
Inadaiwa kuwa vigogo watatu wa mji mdogo wa Mirerani, wamejenga nyumba za
kuishi kwenye eneo hilo na watu wengine zaidi ya 11 wamejimegea viwanja
kiubabe na kujiandaa kujenga ili hali mradi huo unatarajia kuanza kujengwa.
Akizungumza juzi wakati akifungua maonyesho ya madini ya vito ya siku
mbili yaliyofanyika mji mdogo wa Mirerani, Kambona alisema mchakato wa
kuwalipa fidia waliokuwa wanamiliki eneo hilo upo tayari hivyo wavamizi hao
waondoke.
Alisema baada ya kuwalipa waliokuwa wamiliki wa eneo la EPZA, mchakato wa
ujenzi utaanza mara moja kwani kutajengwa kituo kikubwa cha biashara za
kuuza nje ikiwemo soko la madini ya Tanzanite litakalojengwa sehemu hiyo.
Hata hivyo, alipongeza Wizara ya Nishati na Madini kufanya maonyesho hayo
kwa mara ya kwanza kwenye mji mdogo wa Mirerani, sehemu yanapopatikana
madini ya Tanzanite, kwani itasaidia kuboresha soko la madini katika eneo
hilo.
“Ni heshima kubwa tumepatiwa watu wa Simanjiro hususan mji mdogo wa
Mirerani, hivyo tutumie fursa hii kwa wachimbaji kuleta madini yetu kwenye
maonyesho haya ili kuboresha uchumi wetu,” alisema Kambona.
Mmoja kati ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Saniniu Laizer alisema
maonyesho kama hayo yanachangia kutangaza madini hayo, kwani kuna baadhi ya
watu wana dhana potofu kuwa yanachimbwa nchi ya jirani.
“Kupitia maonyesho haya tunaiomba serikali iboreshe zaidi sekta ya madini
ya vito kwa kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo kwani wana changamoto
nyingi zinazowakabili,” alisema Laizer.
Kwa upande wake, kaimu kamishna wa madini kanda ya kaskazini Elias
Kayandabila alisema maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza mji mdogo
wa Mirerani na yanatarajia kufanyika tena mwakani kwenye eneo hilo.
Kayandabila alisema kupitia maonyesho hayo wafanyabiashara wadogo kwa
wakubwa wa madini ya vito ikiwemo Tanzanite, Tomarine ya kijani, Garnet ya
kijani, Roadlite na mengineno, watanufaika nayo kwa kuboresha masoko yao.
Maonyesho hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Nishati na Madini
kanda ya ya kaskazini na vyama vya wachimbaji madini (Remas), chama cha
madalali wa madini (Tasgedo) na chama cha wauzaji wa madini (Tamida).