Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya kutoka Jijini Mwanza, Joseph Stanford, maarufu kwa jina la Rich4D akiwaonyesha wanahabari Jijini Mwanza (hawapo pichani) ramani ya Mkoa wa Dar es salaam aliyoitumia kutambua maeneo ya Mkoani huo.
Hiyo ilikuwa baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuonana na Rais John Pombe Magufuli ili kumpongeza kwa kuwajumuisha wasanii katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika baraza lake la Mawaziri. Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kutimiza adhma yake hiyo.
Msanii Joseph Starnford maarufu kwa jina la Rich4D alitembea kwa miguu kutoka Jijini Mwanza hadi Jijini Dar es salaam ili kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwajumuisha Wasanii katika Baraza lake la Mawaziri, amesisitiza kuwa shauku yake ni kuonana na rais ili kutimiza adhma yake.