Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Makao Makuu
ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma ambapo Mkutano Mkuu unaendelea ni kwamba,
baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo
kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti katika uchaguzi mkuu mwaka
2015.
Miongoni wa waliofukuzwa uanachama ni pamoja na
mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba huku
Adam Kimbisa akisamehewa na Emmanuel Nchimbi akipewa onyo kali. Onyo kali
alilopewa Nchimbi ina maana kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa miaka
minne.
Kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi
nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo
zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika. Hivyo, CCM
italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba
nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae
mwaka huu.
Wengine waliovuliwa uanachama ni Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Kinondoni Madenge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assa Simba,
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya, Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga
Ernest Kwirasa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Nesta Msabatavunga, Mjumbe wa
Halamshauri Kuu (NEC) ya CCM, Ali Sumaye, Mjumbe wa NEC Arumeru, Mathias Manga.
Pia, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido Leiza
amefukuzwa uanachama pamoja na Mwenyekiti wa CCM Arusha Mjini, Saileli Molleli,
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Omary Hawadhi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Muleba, Mwenyekiti wa CCM Babati, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bunda, Mjumbe wa NEC
Gureta.
Waliopewa onyo kali kwa makosa mbalimbali ni
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Ahmed Kiponza ambaye amepewa onyo
kali na kuondolewa madarakani, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Singida, Hassa Mzaha,
Mwenyekiti wa UWT Gezabulu, Mjumbe wa NEC Kilwa, Ali Mchumo na Mjumbe wa NEC
Tunduru, Cheif Kalolo ambaye amevuliwa ujumbe huo na kupewa onyo kali
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia