Katibu tawala
wilaya
ya Iringa Joseph Chitinka akiwasalimia wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup. Katibu tawala
wilaya
ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Katibu tawala
wilaya
ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya kijiji cha Mangalali kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MASHINDANO ya kombe Mbuzi Cup
yatafikia tamati tarehe 30 mwezi wa tatu kwa kuzikutanisha timu za Mkwawa Rangers
na Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na fainal hiyo itachezwa katika kijiji
cha Kalenga kata ya Kalenga wilayani Iringa mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua
vipaji wa wachezaji kata hiyo.
Akishudia mchezo wa nusu
fainal kati ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) na
timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga katibu tawala
wilaya
ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema ni wakati mzuri
kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia
kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo
yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,
"Mashindano haya ni
muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na
kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo
hiyo" alisema Chitinka
Aidha Chitinka aliongeza kwa
kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza
kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa
vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.
“Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua
vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu mbalimbali na lengo likiwa ni
kuhakikisha vipaji vyote vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni
ajira si mnamuana mchezaji Mbwana Samatta”.alisema Chitinka
Mwenyekiti wa Kamati ya
Mashindano hayo Obeid Msigwa aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma
ili ipatikane timu ya bora ambayo itakuwa ikiwakilisha katika mashindano ya mbalimbali.
“Soka imewapa ajira
mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya
kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema Msigwa
Kwa upande wake mlezi wa
mashindano hayo kamanda wa vijana wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya Iringa Jackson
Kiswaga alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia
kukuza mpira wa wilaya ya Iringa.
“Ilani ya chama cha
mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara
kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya
wendawazimu”alisema Kiswaga.
Mashindano ya Mbuzi Cup ni
miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili
kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia