Ticker

6/recent/ticker-posts

HATIMAYE JOHN BARNES AWASILI JIJINI DAR

Akiwa nchini Barnes atafanya mafunzo kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 Serengeti Boys pamoja kuhudhuria fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 ya benki hiyo yatakayofanyika Jumamosi Machi 4. Bingwa wa Mashindano hayo atapata nafasi ya kwenda nchini Liverpool Uingereza.Timu zilizoingia fainali za mashindano hayo ya kikanda ni Azania Group ya Tanzania, Capital FM ya Kenya na Cocacola ya Uganda.
Mchezaji nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes (wa pili kushoto) akiwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere- VIP Terminal I na kupokelewa na wenyeji wake ambao ni Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (wa pili kulia), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba (kulia) pamoja na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas (kushoto).
Mchezaji nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wenyeji wake Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (kulia), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba (wa tatu kulia) pamoja na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere- VIP Terminal II leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa Mchezaji nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mchezaji nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes akionyesha jezi ya Timu ya Taifa kwa waandishi wa habari aliyokabidhiwa na Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mchezaji nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes (katikati) akiongozana na wenyeji wake Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahaman Said (kulia), Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es Salaam.
Mchezaji nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes (wa pili kulia) akizungumza jambo na Meneja wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam-The Kilimanjaro, Timothy Mlay alipowasili kwenye hoteli hiyo jioni hii jijini Dar es Salaam.
Mchezaji nguli wa kimataifa wa Timu Liverpool, John Barnes akisalimiana na mmoja wa mashabiki wa timu ya Liverpool Benjamin Kasenyenda mara baada ya kuwasili kwenye wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam-The Kilimanjaro.

Post a Comment

0 Comments