Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni
mbalimbali zilizofanyika na jeshi hilo kwa wiki moja leo jijini Dar es
Salaam.
Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha dawa za kulevya zilizokamatwa katika
operesheni leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akinyesha gari lililokuwa linatumika kwa ajili ya
utapeli na magari yaliyokamatwa kwa tuhuma mbalimbali leo jijini Dar es
Salaam.
Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha pikipiki zinazopita katika barabara ya
mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi
(CP), Simon Sirro akionyesha bunduki iliyoteleekezwa na watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi leo jijini Dar es Salaan.picha na
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JESHI la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linawashikilia watuhumiwa
wawili wanaojihusisha usambazaji wa dawa kulevya pamoja na utumiaji wa
dawa hizo.
Wanaotuhumiwa
na usambazaji wa dawa za kulevya na utumiaji ni mwanamziki Vanessa Mdee
na Dumisha Heri ambao wamekamtwa na polisi hivi karibuni.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda Polisi wa Kanda
Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro
amesema wasanii hao walikamatwa hivi karibuni katika mazingira ambayo
hakutaja kutokana na masuala ya kiupelelezi.
Amesema kuwa
baada ya kukamilika kwa upelelezi watafikishwa mahakamani kujibu mashataka yanayowakabili.
Wakati huo
huo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wanaojihusisha na utapeli kwa
kutumia vicoba kuhusisha majina ya Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP , Dk.
Reginald Mengi ,Mke wa Rais Mstaa na Mbunge, Salma Kikwete pamoja na
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee.
Amesema kuwa
matapeli hao wametengeneza mtandao wa Focus Vicoba ambao watu wakiingia
katika mtandao huo wanakuta taarifa mbalimbali zikiwemo za viongozi na
watu wenye uwezo wa kifedha kuwa ndio wanaoendesha Vicoba hiyo kwa
kutumia namba za simu za 0757 308381 na 0768 199359 ambazo sio namba za
viongozi hao.
Kamishina
Sirro amesema kuwa mwaka jana walimkamata Boniface Samson Ojwando (27)
kwa tuhuma za kuhusika katika matandao huo na kujipatia fedha kwa njia
za udanganyifu kwa mtandao wa kijamii.
Kamanda
Sirro amesema matapeli wengine walikuwa wanatumia gari zenye namba
usajili T 400 CNC aina ya Toyota Mark II Grand katika maeneo ya Sinza
kwa madai kuwa linauzwa baada ya na baada kukubaliana maziano hufanya
uhalifu wa kupora fadha hiyo iliotaka kununulia gari hilo.
Katika hatua
nyingine jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limekusanya
zaidi ya milioni 840 za makosa mbalimbali ya usalama Barabarani
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia