TIMU YA RIADHA TANZANIA YAKABIDHIWA BENDERA YA NCHI KUWAKILISHA MASHINDANO YA MBIO ZA NYIKA ZA DUNIA YANAYOFANYIKA NCHINI UGANDA MARCH 26

mkuu wa mkoa Simiyu Antoni Mtaka akikabidhi makepteni wa  Timu ya taifa ya
Riadha   leo   rasmi bendera ya Tanzania kwenda
kuwakilisha  nchi katika mashindano ya mbio za nyika  za dunia
yayotarajiwa kufanyika Marchi 26 nchini Uganda ,kapteni wa kike anaitwa  Magdalena Krispini  akiwa mkono wa kushoto ,na kapteni wa kiume  Fabian Josephy akiwa mkono wa kushoto.Na Woinde Shizza,Arusha

Timu ya taifa ya Riadha   leo imekabidhiwa rasmi kupeperusha bendera ya Tanzania kwenda kuwakilisha  nchi katika mashindano ya mbio za nyika  za dunia yayotarajiwa kufanyika Marchi 26 nchini Uganda.

Akikabidhi bendera hiyo , Rais wa shirikisho la Riadha Tanzania ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka  alisema kuwa mashindano haya ni makubwa kidunia  na nchi zipatazo 70  zitashiriki mashindano haya ,pia kutakuwepo na nchi zingine 216 ambazo zitashiriki lakini hazitaleta timu.

Aidha alibainisha kuwa hii ni mara ya kwanza kwa nchi  ya Tanzania baada ya miaka 26 kupita kupeleka timu ambayo imekamilika ikiwa na wachezaji 28 sawa na nchi zingine kama vile Ethiopia,Kenya na Uganda.

“Imepita miaka 26 tangu nchi yetu ya Tanzania ikipeleka  wachezaji wakiwa kamili katika mashindano mbalimbali ,lakini kwa sasa hivi naweza kujivunia kwakuwa tumewafua wachezaji vya kutosha na tumepata timu kamili yenye wachezaji 28 ambao ni sawa na wenzetu wa Kenya na Ethiopia wanavyopelekaga wachezaji ivyo tunaimani kabisa kwa wingi huu lazima tutashinda na medani kurudi hapa nchini”alisema Mtaka

Alisema kuwa  mashindano hayo yanaitaji mchezaji mwenyewe kuondoa tofauti alizonazo na kujituma  zaidi kwani mbali na kuiwakilisha nchi lakini pia akishinda itamsaidia yeye mwenyewe kujinufaisha kwani zawadi zinazotolewa ni kubwa nazinamnufaisha mshindi.
Alisema kuwa wachezaji wamekaa kambini  kwa muda mchache lakini wamejifua vya kutosha  hivyo anaimani kabisa wanapoenda kushindana watashinda .
“Napenda kutumia muda huu kuwashukuru na kuwapongeza shirika la hifadhi ya Taifa (Tanapa) kwa kudhamini safari nzima ,na napenda kuahidia fedha zao hazitapotea bure bali zitawalipa pale wanariadha wetu watakapo rudi na medani ,napenda kuwaambia hakuna mchezo mwingine ambao wanaweza kuutumia kujitangaza zaidi ya riadha”alisema Mtaka

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Tanapa  Nyamakumbati  Mafuru  alisema kuwa wao kama Tanapa wameona michezo ni njia moja wapo  na muhimu ya kutangaza utalii wetu wan chi yetu  hivyo ndio maana tumeona tutumie fursa hii iliyojitokeza

“Unajua mashindano haya yanauthuriwa na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali hivyo tumeona ni njia moja wapo ambayo tutaitumia kutangaza vivutio vilivyopo katika nchi yetu na ndio maana tumeamua kudhamini kuwapeleka timu hii ya taifa Uganda  ili wakatuwakileshe na kututangaza pia “alisema Mafuru

Naye katibu mkuu wa shirikisho la Riadha Gida Bidai alisema kuwa  timu ya taifa imeondoka na wachezaji 28 pamoja na viongozi wake wote wakiwa salama na anaamani wataenda kuwaletea ushindi  huko waendapo kwani wamefanya mazoezi ya kutosha

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.