Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA YAOBWA KUTANGAZA MADINI YA TANZANITE

Makamu wa Rais wa Simba SC Jofrey Nyang Kaburu akizungumza na wakurugenzi wa
kampuni ya TanzaniteOne, Hussein Gonga (kulia) na Faisal Shabhai
walipokuwa Mazuru Grand Hotel Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro
Mkoani Manyara, baada ya timu hiyo kutembelea migodi ya madini ya
Tanzanite.
Na Woinde Shizza,Mererani
Kampuni ya madini ya TanzaniteOne imeuomba uongozi wa timu ya soka ya
Simba SC kuyatangaza madini ya Tanzanite ambayo duniani yanapatikana
pekee mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ili
yaweze kupata soko zaidi.

Mkurugenzi wa kampuni ya TanzaniteOne Hussein Gonga akizungumza juzi baada
ya viongozi na wachezaji wa timu hiyo kutembelea migodi alisema Simba
ina uwezo mkubwa wa kuitangaza Tanzanite.

“Kupitia nafsi hiyo tutapata nafasi kubwa ya kujitangaza kwani Simba
ni timu kubwa na ina marafiki wengi ndani ya nchi na nje ya nchi na
naamini kampeni hii itakuwa na mafanikio makubwa,” alisema Gonga.

Alisema wachezaji na viongozi wa timu hiyo kwa nafasi yao wana uwezo
mkubwa wa kuyatangaza mafanikio yaliyopatikana kupitia madini ya
Tanzanite, ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya TanzaniteOne Faisal Shabhai
akizungumza akiwa Mazubu Grand Hotel mji mdogo wa Mirerani ambapo timu
ya Simba ililala alisema ziara hiyo itakuwa na mafanikio makubwa.

Shabhai alisema kupitia nafasi hiyo timu ya Simba itayatangaza vya
kutosha madini ya Tanzanite ambayo kwa namna ya pekee imeyabadili
maisha ya wananchi wa eneo hilo na serikali kupata kodi yake.

Makamu wa Rais wa Simba Jofrey Kaburu alisema ziara hiyo itawanufaisha
viongozi na wachezaji ambao walikuwa hawajawahi kutembelea migodi na
kujionea madini ya Tanzanite yaliyovyo.

Kaburu alisema Tanzanite ni kitu muhimu kwenye jamii na
watawafahamisha watanzania na kuwaelimisha madini hayo kwa hapa
duniani yanapatikana kuwa Mirerani pekee hivyo ni jambo la kujivunia.

“Mji wa Mirerani hivi sasa umeendelea tofauti na awali tulivyokuja
miaka mitano iliyopita kwani tumeona maendele mengiikiwemo Mazuru
Grand Hotel ambapo timu yetu ilifikia,” alisema Kaburu.

Alitoa pongezi kwa uongozi wa kampuni ya TanzaniteOne ambayo
inamilikiwa na wazawa kwa kutoa ajira kwa wananchi na kuendesha
ipasavyo mgodi huo huku ikilipa kodi kwa serikali.

Baada ya kumaliza kutembelea machimbo madini kwenye kampuni ya
TanzaniteOne, timu ya Simba ilicheza mchezo wa kirafiki na timu ya
Mirerani Stars kwenye uwanja wa barafu Mirerani na kushinda bao 1-0
lililofungwa na Mwinyi Kazimoto.

Post a Comment

0 Comments