Mtu Mmoja Aburuzwa na Pikipiki Barabarani Akidhaniwa Kuwa Mwizi, Afariki
Mtu moja ambaye jina lake hajijafahamika ameuawa na wananchi wenye hasira kali huko maeneo ya kwa Mrombo Jijini Arusha ,akidhaniwa kuwa ni mwizi wa pikipiki baada ya mtu huyo kupita na kufananishwa na waendesha pikipiki hao.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa majira ya saa saba mchana wananchi hao walimuona mtu huyo wakadhania kuwa ndiye aliyewahi kumnyang'anya mwenzao pikipiki hivyo wakaanza kumshambulia na kumburuza ambapo hadi jeshi la polisi kufika eneo la tukio mtu huyo
alikuwa tayari ameshachoka na hali yake ilikuwa mbaya wakiwa njiani kumpeleka hospitali alifariki.

Kamanda Charles Mkumbo amewataka wananchi kutochukua sheria mkononi kwani wanaweza kumdhuru mtu ambaye hausiki na tukio amesema kuwa wanapomuhisi mtu kuwa ni muhalifu watoe taarifa kwa jeshi la polisi ili sheria ichukue mkondo wake. 


Hadi sasa 
jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu watano ambao ni 
waendesha pikipiki kwa kuhusika katika tukio hilo,mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika hospitali ya maountmeru ukisubiria ndugu na jamaa 
kwenda kumtambua

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.