Meneja wakala wa barabara Mkoani Tanga (Tanroad) Mhandisi Alfred Ndumbaro akisisitiza jambo kwenye kikao hicho kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu |
Meneja wa Temesa Mkoa Mhandis Margareth Gina akitolea ufafunzi baada ya maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa kikao hicho |
Wajumbe wakifuatilia hoja
zilizoainishwa kwenye makabrasa kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi
(CCM) Omari Kigua na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Sauda
Mtondoo
Mbunge wa Jimbo la
Pangani (CCM) Jumaa Aweso akifuatilia jambo kwenye kabrasha lake
wakati kikao hicho kikiendelea
Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias
Mwilapwa akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga
Daudi Mayeji katika wakati wa kikao hicho
Mkurugenzi wa Halmashauri
ya wilaya ya Lushoto,Kazimbaya Makwega akiperuzi kabrasa kwenye kikao
hicho
Mbunge wa Jimbo la Tanga
(CUF) Musa Mbaruku na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (Chadema)
Yosepher Komba
Mbunge wa Jimbo la
Mkinga(CCM) Dustan Kitandula kushoto akiwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri hiyo Rashid Gembe
Mkuu wa wilaya ya Handeni
Godwin Gondwe akifuatilia kwa umakini kikao hicho
kulia ni Mbunge wa Jimbo
la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akifuatilia kikao
hicho
Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mkoani Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akifuatilia kwa umakini kikao
hicho
Mwandishi Mwandamizi wa
Shirika la Utangazaji la TBC Mkoani Tanga,Bertha Mwambela akiandaa
taarifa za kikao hicho
WAKALA wa Ufundi na Umeme Mkoani
Tanga (Temesa) wameagizwa kuwasilisha orodha ya majina ya wadaiwa sugu
wa taasisi mbalimbali za serikali kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine
Shigella ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa ikiwemo
kuharakisha ulipwaji wake.
Agizo hilo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela wakati wa kikao cha kwanza cha Bodi ya barabara mkoani hapa ambapo alisema wao kama serikali ya mkoa hawapo tayari kuona wakala huyo akishindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo kutokana na juhudi zao kurudishwa nyuma kimaendeleo.
Katika kuhakikisha suala hilo linapata mafanikio makubwa yenye tija alimtaka Meneja wa wakala wa Ufundi na Umeme (TEMEMSA) Mkoa Tanga, Mhandisi Margareth Gina kumpelekea idadi ya wadaiwa sugu na taasisi hiyo ili kuweza kuangalia namna ya kuweza kupata malipo yao.
Hatua hiyo inafuatia taarifa ya Meneja wa Temesa Mkoa kuonyesha zipo taasisi nyingi za Serikali zinazodaiwa fedha nyingi bila kuwepo jitihada zozote za ulipwaji wa madeni hayo huku tasisi hizo zikiendelea kupatiwa huduma na taasisi hiyo ya Serikali.
Alisema ifike wakati kwa taasisi zote za umma zinazopata huduma kutoka kwa wakala huo wa ufundi na umeme wahakikishe wanalipa madeni yao kwa wakati kabla majina hayo ya wadaiwa hao sugu hayaja wekwa hadharani.
Mkuu huyo alisisitiza umuhimu wa majina ya wadaiwa wote sugu
yaorodhoshwe bila ya kuoneana aibu na taasisi za Serikali ambazo inadaiwa kuwa ndio vinara wakubwa wa kudaiwa ili kuweza kuangalia namna ya kupunguza madeni hayo ambayo ni hatari kwa ukuaji wa wakala huyo.
Awali akizungumza katika kikao hicho,Meneja wa Temesa Mkoa Mhandis Margareth Gina alisema temesa imekuwa ikitoa huduma bora kwa taasisi za Serikali kutokana na kuwepo na wataalamu wengi waliobobea katika fani mbalimbali huku wakishindwa kufikia malengo kutokana na kutolipwa
na wateja wao.
Mhandisi Gina alisema ipo orodha kubwa ya majina ya wadaiwa sugu ambapo ipo haja ya kuyaweka hadharani kama Mkuu wa Mkoa alivyoagiza na kufanya hivyo kunaweza kusaidia kwa namna moja au nyingine kuweza na kukusanya madeni hayo.
“Zipo taasisi za serikali zanadaiwa hadi milioni 100 na orodha yote ya wadaiwa sugu ninayo na naweza kuyataja ila naona itakuwa kufedheheshana tu mbele ya kikao hiki”Alisema
Aidha alisema taasisi za Serikali kwa asilimia kubwa zimekuwa miongoni mwa wateja wanaoikwamisha temesa kuendelea na ufanisi wa shughuli zake jambo ambalo linatakiwa litafutiwe ufumbuzina wa haraka kukomesha tabia hiyo iliyozoeleka.
Kwa upande wake, katibu Tawala Mkoa Tanga Mhandisi Zena Saidi alisema hakuna sababu ya kuficha wanaodaiwa lazima waorodheshwe na walipe madeni yao kwa wakati ili temesa iweze kuendelea na majukumu yake.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia