Shindano la kumsaka Tanzania Miss super Model linatarajiwa kufanyika mapema mwezi marchi 31 mwaka huu katika ukumbi wa hotel ya Mounti Meru uliopo ndani ya jiji la Arusha
Akiongea na waandishi wa habari muaandaaji wa shindano hilo Ibra Thabit alisema maandalizi yamekamilika na hadi sasa warembo wote wanaoshiriki shindano hilo wako kambini kwa ajili ya mazoezi
Alisema kuwa jumla ya warembo 14 kutoka mikoa yote ya Tanzania watashiriki shindano hili na mshindi atakae patikana ataenda kuwakilisha mashindano ya Dunia Miss Top Super Model yanayotarajiwa kufanyika nchini china
washiriki wa shindano la Tanzania Miss super Model wakiwa katika picha ya pamoja katika hotel moja iliopo katika mji mdogo wa mererani wakati walipo fanya ziara katika mji huo
mkurugenzi wa Mnyalu intatament Charles Endru akiwa pamoja na warembo wa Tanzania miss super model