Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza katika kikao cha kamati ya Utekelezaji kilichoketi mapema ya leo kabla ya kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Sadifa Juma Khamis wa pili kulia akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipowasili katika kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.
Mwenyekiti Wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg:Sadifa Juma Khamis akifungua Kikao cha Baraza Kuu Maalum la UVCCM Taifa kilichofanyika Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Mohammed Seif Khatibu Akizungumza katika kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Uvccm Taifa Sadifa Juma Khamis wa pili kulia akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipowasili katika kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma.
Mwenyekiti Wa UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Ndg:Sadifa Juma Khamis akifungua Kikao cha Baraza Kuu Maalum la UVCCM Taifa kilichofanyika Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Mohammed Seif Khatibu Akizungumza katika kikao cha Baraza kuu Maalum la Uvccm Taifa lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma leo.
Ndg:Nyundo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM kupitia UVCCM akichangia hoja katika kikao cha Baraza kuu Maalum Kilichofanyika leo Mjin Dodoma.
Mhe: Deo Ndenjembe Mkuu wa Wilaya ya Kongwa akichangia hoja katika kikao cha Baraza kuu Maalum Kilichofanyika leo Mjin Dodoma.
Wajumbe Wa Baraza kuu la UVCCM Taifa
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mariam Ditopile akisikiliza kwa Makini
Wajumbe Wa Baraza kuu wakiwa kikaon
SOMA
MAAZIMIO
YA BARAZA KUU MAALUM LA UMOJA WA VIJANA WA CCM TAIFA LILILOKUTANA ALHAMIS
TAREHE 9/03/2017 ROYAL VILLAGE HOTEL MJINI DODOMA
Umoja
wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo Alhamis tarehe 9/03/2017 umefanya kikao cha Baraza
Kuu la UVCCM Taifa Maalum chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Sadifa Juma Khamis
(MCC)(MB) katika Hotel ya Royal Village Hotel Mjini Dodoma.
Kikao
kwa kauli moja kimepitisha na kuridhia mapendekezo ya Marekebisho ya Kanuni ya
Umoja wa Vijana wa CCM kufuatia maboresho ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi
Toleo la 1977 marekebisho ya 2017 na kupeleka katika Vikao vya Chama Cha
Mapinduzi Taifa kwa hatua zinazoendelea.
“Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itakuwa na uwezo
kwa kushauri, kutoa maagizo ya jumla na maelekezo maalum kwa Jumuiya
zinazoongozwa na CCM”.
“Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa itathibitisha Kanuni/Katiba ya kila Jumuiya inayoongozwa na
CCM marekebisho yake kabla ya kutumika”. Katiba ya CCM ya 1997 Toleo la 2012
uk. 191 kifungu (4) na sura ya (5).
Kufuatia
kikao Maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa
CCM na kuzingatia mambo yafuatayo:-
Mabadiliko
ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake yana lengo la kukiimarisha Chama chetu
ili kuzidi kuziteka hisia, mioyo na fikra za Watanzania walio wengi kwa nia ya
kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika lengo lake la kushika dola na kuleta
maendeleo endelevu.
Kupunguza idadiya wajumbe ili kuwa na michango makini
kwenye vikao vyetu ili kuweza kuwajengea na kuwatetea Vijana wakulima na
wafanyakazi na wale walio katika sekta binafsi ili wanufaike na masuala ya
Kiuchumi, kijamaii na Kisiasa kulingana na fursa zilizopo kama zilivyoainishwa
na kuelekezwa na sera za CCM katika misingi ya kujitegemea.
Mabadiliko
haya yatasaidia sana kupunguza migogoro isiyo na msingi katika Jumuiya
inayotokana na Vikao vya Kikanuni.
Aidha
Umoja wa Vijana wa CCM unaahidi kwa CCM kufanyia kazi maagizo na maelekezo yote
yatakayotolewa kwa lengo la kufikia kwa vitendo dhana ya CCM mpya, Tanzania
mpya wakati Jumuiya hiyo ikielekea kutimiza miaka 40 toka kuzaliwa na kumepiga
hatua kubwa za mafanikio Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa.
Mwisho UVCCM imempongeza
kwa dhati Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli kwa umakini, uhodari, ushupavu na kusimamia vyema Ilani ya
Uchaguzi wa CCM sambamba na azma yake ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi na
Jumuiya zake.
PICHA NA FAHADI SIRAJI
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia