![]() |
picha na maktaba Mchoro unaoonyesha mapafu ya mwanadamu yaliyoathiriwa na maradhi ya Kifua Kikuu. |
Na Woinde Shizza ,monduli
Udogo wa madirisha yanayojengwa katika jamii ya kifugaji,unywaji maziwa mabichi na kula ugolo na baadhi ya mila imekuwa ni mojawapo za sababu zinazopelekea ugonjwa wa kifua kikuu katika jamii ya kifugaji sambamba na uvutaji wa sigara.
Kuwepo kwa madirisha madogo kunasababisha hewa kutozunguka na kutoka nje hali ambayo imekuwa inahatarisha wakazi wa nyumba hizo hasaa jamii za kifugaji na kuwataka kubadili ujenzi wa nyumba zao.
Hayo yameelezwa leo na Mganga mkuu wa hospitali ya kanda ya kijeshi ya chuo cha mafunzo ya kijeshi Monduli(TMA) Kapteni dr,Is-haka shekue wakati wa maadhimisho ya ugonjwa wa kifua kikuu ambayo yalienda sambamba na upimaji kwa wananchi ambayo yalifanyika katika viwanja vya soko alhamisi iliyoko katika wilaya ya monduli katika mkoa wa Arusha.
Ambapo zoezi hilo limeendeshwa na Jopo la madaktari bingwa wa magonjwa ya binadamu kutoka chuo cha
mafunzo ya kijeshi monduli(TMA) wameendesha zoezi la kupima magonjwa ya
kifua kikuu na ukimwi bila malipo kwa watu wa jamii ya kifugaji
wilaya ya monduli huku kukiwa na mwitikio mkubwa wa watu
waliyojitokeza kwenye zoezi hilo ili kupima afya zao pamoja na ugonjwa wa ukimwi.
Mganga mkuu wa hospitali ya chuo cha mafunzo ya kijeshi kapteni
is-haka shekue amesema kuwa wamelazimika kuendesha zoezi hilo baada
ya uwepo wa ongezeko kubwa la watu wanaoambukizwa kifua kikuu kwa
watu wa jamii ya kifugaji unaosababiswa na mazingira wanayoishi.
Aliongeza kuwa hivi sasa wanaendelea kuwafatilia hadi majumbani kwao wagonjwa wa kifua kikuu ili kuhakikisha wanaweza kuendelea na matibabu yao kwa muda waliopangiwa kwani dozi yake niyakuanzia miezi mitatu hadi sita itategemea hali ya mgonja husika.
Pia wanaendelea na uhamasishaji na ameongeza kuwa zoezi hilo ni ednelevu na mara baada ya maadhimisho ya leo kuisha wataendesha zoezi hilo katika hospitali yao iliyoko katika eneo la kambi ya kijeshi monduli (tma).
Kwa upande wake mratibu wa kifua kikuu na ukoma wilaya ya monduli dk godson
lekasiye amesema maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu yanaongeka
kwa kasi kubwa katika wilaya hiyo ambapo takwimu zinaonyesha kuwa 2014 wagonjwa walikuwa ni 346 na mwaka 2015wagonjwa walikuwa 351 na takwimu za mwaka huu2016 wagonjwa wako zaidi 422 hadi sasa .
Ambapo eneo linaloongoza kwa maambukizi hayo ni eneo la mto wa mbu ambapo wameweka mikakati madhubuti ili kuweza kukabiliana na ongezeko la ugonjwa huo.
Kwa upande wake mmoja wa muathirika wa ugonjwa wa kifua kikuu George joseph alisema kuwa amepata maambukizi hayo tangu mwaka jana ambapo kwa sasa anaendelea na dozi yake ya miezi sita amewaomba watalaam kufanya kampeni
endelevu ya kutoa elimu ya kuepuka maambikizi kwa watu wanaoishi
maeneo ya vijijini ambako kuna waathirika wengi zaidi