WATANZANIA wamepata nafasi ya kuwakilisha Afrika Mashariki katika uwanja wa mpira wa Anfield unaotumiwa na Liverpool baada ya timu iliyokuwa inawakilisha ya Azania Group kutwaa ubingwa wa Standard Chartered 2017.
Katika michuano hiyo iliyohusisha klabu zilizoingia fainali kutoka Tanzania, Kenya na Uganda mwakilishi wa timu ya Liverpool mchezaji Gwiji John Barnes na mabalozi wa Uingereza, Uganda na Kenya, Azania ilionesha kandanda safi .
Azania imepata nafasi ya kutwaa kombe hilo katika Mashindano hayo ambayo yanajulikana kama ‘Standard Chartered-Road to Anfield Tournament’ kwa tofauti ya magoli katika kipute ilichokipiga na Capital FM katika viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam jana.
Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande (kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya JK Youth Park na kupokelewa na Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (katikati) wakati wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.(Picha zote na thebeauty.co.tz)
Azania Group of Companies ambayo ilikuwa inawakilisha Tanzania ilijikusanyia pointi saba kama ilivyokuwa Capital FM kutoka Kenya lakini waliweza kupata nafasi kutokana na kujipatia magoli matatu zaidi dhidi ya Kenya ambao walikuwa na magoli mawili.
Mpira huo ambao ulichezwa kwa dakika tano kila upande ulikuwa mkali na ambao ulishindwa kutoa utabiri wa wazi nani ataibuka mshindi na hivyo kupata nafasi ya kuingia uwanja wa Anfield Mei mwaka huu kuangalia mechi za Liverpool.
Baada ya kila timu kuicheza mechi tatu katika raundi ya kwanza na kila mmoja kujipatia pointi tatu waliingia katika raundi ya pili.
Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande (mwenye kofia) akizungumza na timu ya Capital FM baada ya kuwasili kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Katika michuano hiyo Coca cola ya Uganda ilicheza dhidi ya Azania Group of Companies na kuondolewa mapema katika michuano hiyo pamoja na watu wake kuwa na miili ya soka.
Kutokana na Uganda kuondolewa mapema, Azania waijikuta wakikabiliana na washindi wa mwaka uliopita mabingwa wa Kenya.
Kenya walicheza mpira ambao ulileta taabu sana, mpira wa kujihami na hivyo kutibua mbinu waliyokuwa nayo Azania ambao walitaka kumaliza game mara moja.
Unaweza kusema kwamba kipa wa Capital FM’s, Shafi Sudi ndiye alikuwa staa wa mechi kutokana na kufanikiwa kuzuia kasi ya mashambulizi kutoka Azania yaliyokuwa yakiongozwa na Nahodha Shabaka Hamis.
Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha (mwenye tisheti nyeupe) akizungumza na timu ya Coca cola kutoka Uganda mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya JK Youth Park kushuhudia fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.
Kutokana na fainali hizo kutokuwa na mfumo wa penati timu ambayo inamaliza gemu ikiwa na pointi zaidi huwa ndio washindi na katika hilo Watanzania ndio wawakilishi wa timu za Afrika Mashariki katika uwanja wa Anfield.
Kutokana na ushindi huo Capital FM wanakuwa wa pili na nafasi ya tatu inashikwa na Coca cola ya Uganda.
Akizungumza baada ya gemu kumalizika, Rajab Ali ambaye ndiye aliyeibeba Azania Group alisema kwamba alikuwa na furaha kubwa kwenda kuishuhudia Liverpool FC ikikipiga katika uwanja wa Anfield kwani ndilo ilikuwa nia yao kubwa.
Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes (katikati) akiwasili pamoja na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kushoto) na kupokelewa na Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba walipowasili kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Naye nahodha wa Capital FM, Lassie Atrash alisema kwamba wameshindwa kufanya vyema kwa kuwa uwanja ulikuwa mdogo.
Hata hivyo alisema ulikuwa ni mchezo safi na mshindi ilikuwa lazima apatikane na kusema kwamba ana matumaini kuwa Azania itawawakilisha vyema Afrika Mashariki huko England.
Awali mchezaji John Barnes akizungumza kabla ya michezo hiyo alisema anafurahishwa na kutambua kwamba soka linatengenezwa Afrika Mashariki na hivyo kuondoa dhana potofu kwamba soka katika Afrika linapatikana Afrika magharibi pekee.
Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes akitambulishwa kwa Mwakilishi wa Balozi wa Uingereza, Daniel Rathwell alipowasili kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba.
Alisema kwamba amefurahishwa na kuona kwamba Liverpool imepata mashabiki wengi kutoka Afrika ambao wanatengeneza familia ya timu hiyo katika sera iliyoanzishwa miaka ya 1960 ya kuwa na wapenzi na mashabiki wa damu wa timu hiyo.
Aidha alizungumzia uhusiano wao na walezi Standard Chartered na kutabiri kwamba Tanzania itaibuka washindi kutokana na yeye kuwapo Kenya mwaka uliopita na Kenya kufanikiwa kwenda England kuishuhudia Liverpool.
Pamoja na mchezaji huyo mahiri wa zamani wa Liverpool kuzungumza katika fainali za tuzo hizo, wapenzi wa michezo pia walipata kusikia nasaha kutoka kwa Balozi wa Uingereza nchini, Balozi wa Uganda na mwakilishi wa Kenya.
Meza kuu kwenye fainali za mashindano ya Standard Chartered Road to Anfield 2017, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine, Mwakilishi wa Balozi wa Uingereza, Daniel Rathwell, Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani, Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha pamoja na Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande.
Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes akiwasalimia washiriki wa fainali mashindano hayo ya Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyomalizika jana jijini Dar es Salaam.
Timu ya Coca cola Uganda ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza fainali za mashindano hayo.
Timu ya Capital FM kutoka Kenya ikiimba wimbo wa Taifa kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha timu ya Azania Group of Companies wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 zilizofanyika kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kulia) akishiriki kuimba wimbo wa taifa na vijana wake kabla ya kuanza kwa fainali za mashindano hayo.
Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha katika picha ya pamoja na timu ya Coca cola kutoka nchini Uganda.
Meza kuu ikisalimiana na wachezaji na kuwatakia kheri ya mchezo mwema.
Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande katika picha ya pamoja na timu ya Capital FM kutoka Kenya.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akijumuika na wadau wa soka kupasha misuli moto kabla ya kuanza kwa mechi za fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika viwanja vya JK Youth Park.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (kulia) akibadilishana mawazo na Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes wakati wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya JK Youth Park.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akizungumza na wageni waalikwa pamoja na washiriki wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017.
Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande akitoa salamu kwa washiriki wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika viwanja vya JK Youth Park.
Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha akiwasalimu washiriki wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 katika viwanja vya JK Youth Park.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Uingereza, Daniel Rathwell akizungumza kwa niaba ya balozi wake kwenye fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield yaliyofanyika katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesiga Celestine, akitoa salamu za TFF kwa wageni waalikwa na washiriki wa fainali za mashindano hayo.
Wafanyakazi wa Standard Chartered Bank na wadau wa soka waliohudhuria fainali za mashindano hayo.
Mtendaji Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kulia) akitazama vijana wake walipokuwa uwanjani.
Benji la ufundi la Azania Group of Companies.
Mechi ya utangulizi kati ya mashabiki wa timu ya Liverpool (tisheti nyeupe) na wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered (vesti nyekundu) ambapo mashabiki wa timu ya Liverpool waliinyuka benki hiyo bao 1-0.
Kiungo wa timu ya Azania Group of Companies, Rajabu Ali akiwatoka wachezaji wa timu ya Coca cola kutoka Uganda.
Nahodha wa Capital FM, kutoka Kenya, Lassie Atrash akizungumzia mchezo ulivyokuwa kwa wanahabari mara baada ya fainali hizo kuisha na Tanzania kuchukua ubingwa.
Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda (kulia) na watoto wake katika picha ya pamoja na Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Liverpool wakiimba wimbo "You'll never walk alone" pamoja na Gwiji huyo John Barnes.
Mbunge wa Mbinga Mjini, Sixtus Mapunda (katikati) akikabidhi zawadi kwa mmoja wa waamuzi wa fainali za mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017 yaliyofanyika jana katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akiushuhudia tukio hilo.
Mwakilishi wa Balozi wa Kenya nchini, George Alande akiwavisha medali washindi watatu timu ya Coca cola ya Uganda katika mashindano ya Standard Chartered road to Anfield 2017. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akiushuhudia tukio hilo.
Picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo.
Balozi wa Uganda nchini, Mh. Dorothy Samali Hyuha akiwavisha medali washindi wa pili wa Standard Chartered road to Anfield 2017 timu ya Capital FM kutoka Kenya. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (wa pili kushoto) na Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa benki hiyo, Juanita Mramba wakiushuhudia tukio hilo.
Picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo.
Picha ya pamoja na washindi wa pili wa mashindano hayo timu ya Capital FM kutoka Kenya.
Mchezaji maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes akimvisha medali Nahodha wa Azania Group, Shabaan Hamis baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa 2017. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani.
Mchezaji maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (kulia) akikabidhi kombe kwa timu ya Azania Group of Companies kutoka Tanzania, ambao ni mabingwa wa mashindano ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 jijini Dar es Salaam jana.Pamoja naye ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sanjay Rughani (aliyezibwa).
Mchezaji maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (katikati) akiselebuka pamoja na wachezaji wa timu ya Azania Group kutoka Tanzania, mara baada ya kuikabidhi kombe la ubingwa wa mashindano ya Benki ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 jijini Dar es Salaam jana. Pamoja naye ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sanjay Rughani (aliyezibwa).
Mchezaji maarufu wa zamani wa timu ya Liverpool John Barnes (katikati) akifurahi pamoja na viongozi na wachezaji wa timu ya Azania Group kutoka Tanzania (walioko mstari wa nyuma) mara baada ya kuikabidhi kombe la ubingwa wa mashindano ya Benki ya Standard Chartered road to Anfield mwaka 2017 jijini Dar es Salaam jana.Wengine pichani ni Mkuu wa Uhusiano na Masoko Juanita Mramba (wa pili kushoto), Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Sanjay Rughani (wa tatu kushoto), Balozi wa Uganda nchini Mh. Dorothy Hyuha, (wanne kushoto) na Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda na Mtendaji Mkuu wa Azania Group of Companies, Fuad Edha Awadh (kushoto).
Abdullah Zulu Lyana (katikati) katika picha ya pamoja na mashabiki wenzake wa timu ya Liverpool.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia