· Tigo na Ericson wazindua maeneo ya kwanza ya 3G katika miundombinu ya ushirikiano ya GSMA inayojielekeza kuunganis ha maeneo ya vijijini nchini Tanzania.
· Mfumo wa Redio wa Ericsson kwa mara ya kwanza utawapatia wateja huduma bora ya mtandao wa simu, huduma iliyo na ubora ambayo kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imekuwa ikiitoa kwa wateja mbalimbali.
· Katika ushirikiano huu, kampuni ya Tigo itakuwa na asilimia 40 katika uendeshaji wa mtandao.
Ericsson (NASDAQ:ERIC) na mtandao wa simu unaoendeshwa Tanzania Tigo wameungana katika kuzindua maeneo ya minara ya mfano katika maeneo ya vijijini itakayotoa huduma za simu kwa maeneo ya Chiwale na Mingumbi katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambayo yamo ndani vijijini na awali yalikuwa hayajaunganishwa.
Shughuli hiyo ni mwanzo wa miundombinu ya mfano ya kushirikiana kunakofanywa na GSMA pamoja na Tigo, serikali ya Tanzania na waendeshaji wawili wakubwa wa mtandao wa simu kwa kuunganisha zaidi ya watu binafsi zaidi ya milioni 13 wanaoishi sehemu za maeneo ya vijijini hapa nchini.
Miundombinu ya kushirikiana na kuihusisha serikali katika kupunguza kodi katika mikoa hiyo kunawaruhusu waendeshaji kupunguza gharama za kuendesha mitandao mipana katika maeneo ambayo awali ilikuwa haifikiwi na huduma za simu.
Tigo na Ericson zimetoa nafasi katika ushirikiano huu kwa kuzindua eneo la kwanza linalofanya kazi kwa kutumia mfumo wa Redio wa Ericson wa kizazi kipya wenye viwango vingi. Seti hiyo ya suluhisho inawezesha kuwepo kwa uwezo unaotakiwa katika kupunguza gharama za jumla za umiliki hadi asilimia 40 pindi eneo la suluhisho la jumla kwa uwanda mpana wa simu wa Ericsson utakapoanza kufanya kazi. Hii inafanya uwekezaji unaokuwepo katika masoko kuwa na wastani wa chini wa mapato kwa kila mtumiaji.
Suluhisho hili litaiwezesha Tigo na washirika wake kuweza kuyabaini kwa urahisi maeneo yasiyo na huduma katika mkoa, kuharakisha kuanzisha au kuboresha uzoefu wa watumiaji wengine wa uwanda mpana wa simu ndani ya jamii hizi za vijijini. Huu ni uzinduzi wa kwanza kibiashara kwa suluhisho hilo katika Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara.
Fundi Mkuu na Ofisa wa Teknolojia ya Habari, Jerome Albou wa Tigo Tanzania alisema, “ndani ya Tigo ni dira yetu kuongoza katika kupokea intaneti na mtindo wa maisha ya kidijitali nchini Tanzania. Kufikiwa kwa uwanda mpana wa simu za mkononi kutazifungua jumuia hizi za vijijini katika huduma ambazo awali walikuwa hawazipati kama vile huduma ya fedha kwa njia ya simu, huduma za afya kielektroniki, elimu kielektroniki, na serikali mtandao, hivyo kubadilisha namna ambavyo watu wanacheza, kujifunza na kufanya biashara kwa ujumla”.
Mkuu wa Ericsson Kanda ya Afrika, Kusini mwa jangwa la Sahara Jean-Claude Geha, alisema; “Sisi ni wapiga mbiu vinara wa mchango wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kuwezesha utambuzi wa seti mpya na za jumla za Malengo Endelevu ya Milenia (SDGs). Washirika wetu kwa pamoja wanatafuta masuluhisho ya kuleta faida zinazopatikana katika teknolojia ya simu za mkononi kwa kila mtu kwa kuunda ulimwengu ambao ni endelevu na jumuishi zaidi”.
Muunganiko huo mpya wa suluhisho unajumuisha; program ya Ericsson inayosimamia eneo, pamoja na program ya kudhibiti eneo, ambavyo ni Redio 2219, Redio iIiyounganishwa na Antenna, AIR 2488, MINI-LINK 6363, MINI-LINK 6651 ambacho ni kifaa cha ndani na nyongeza mpya kwa ajili ya kuunganisha mitambo hii ya Ericsson. Hali kadhalika inajumuisha programu mpya iliyoboreshwa katika Zero Touch WCDMA na masuluhisho ya mtiririko wa watumiaji.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia