MEYA WA JIJI LA ARUSHA CALIST LAZARO AMPONGEZA MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA KWA KUFANIKISHA KUJENGA VYUMBA VYA MADARASA

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia akiongea na waandishi wa habari

Na Woinde Shizza,Arusha
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia, timu ya wataalam wa Jiji hilo pamoja na baraza la madiwani kwa kufanikisha zoezi la kujenga vyumba vya madarasa, madawati kwakutumia mapato ya ndani pasipo kuchangisha wananchi 
Pongezi hizo zilitolewa juzi Jijini hapa kwenye Baraza la Kawaida la Madiwani lililoshirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali pamoja na wananchi wa Jiji la Arusha.
Lazaro alisema  Jiji limefanikiwa kuondoa kero ya uhaba wa dada rasa, madawati bila kuwachangisha wananchi ,jambo ambalo limesaidia wanafunzi kuanza masoma kwa wakati.
Alisema watoto wote wa shule za msingi wameweza kuingia shuleni na kukaa kwenye madawati kwani Jiji wamefanikiwa kujenga madarasa 56,madawati 1250,madarasa 25 ya sekondari pasipo kuomba fedha sehemu nyingine pamoja na kuwachangisha wazazi.
"Tunakupongeza wewe Mkurugenzi wa Jiji letu pamoja na timu ya wataalam wa Jiji pamoja na madiwani kwa kuhakikisha Jiji la Arusha linaondokana na kero ya uhaba huo wa madawati ambao awali ulikuwa ukisumbua wanafunzi "
Naye Mkurugenzi wa Jiji hilo, Kihamia alishukuru kwa baraza hilo kutambua kazi anazozifanya za maendeleo na kuomba ushirikiano zaidi kwa madiwani hao ili kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wananchi.
Katika baraza hilo Pia kulikuwa na wawakilishi wa idara za serikali walioalikwa ili kutoa taarifa za utendaji kazi kwa baraza hilo ndipo hoja za tatizo la maji ilipoibuka kutoka kwa madiwani ambao walisema inashangaza Jiji la Arusha kuwa ni Jiji la Kitalii lakini bado wananchi wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji huku wengine wakikosa kupata maji na bili kuwa kubwa.
Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Taka  (AUWSA) Mhandisi, Ruth Koya  alisema mamlaka hiyo inashughulikia kero hiyo ya maji na kutoa rai kwa wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka hiyo ili kuweza kutatua changamoto ya maji Jiji la Arusha
Pia suala  la ukodishwaji maduka ya biashara liliibuliwa na madiwani  katika maswali ya papo kwa papo kwa Meya na Mkurugenzi kuwa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo anangilia mchakato wa utoaji zabuni za maduka . ambapo Mkurugenzii wa Jiji , Kihamia alilazimika kukanusha uzumi huo kwa kusema kuwa Rc, Gambo anaweza kuingilia maamuzi ya baraza hilo kwa maslahi ya mkoa kwa mamlaka aliyonayo.
Pia alisisitiza kuwa Rc Gambo alikutana na wajenzi hao wa maduka na wafanyabiashara ili kujua changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa maslahi mapana ya maendeleo.
 Awali Jiji la Arusha liliingia katika mvutano wa wafanyabishara waliopangisha katika majengo ya jiji tatizo liliopatiwa ufumbuzi na Mkuu wa Mkoa hivi karibuni.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.