Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe:Antony Mtaka akizungumza na Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Mapema
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akikagua Banda na kupata
Naelezo Mbali mbali juu ya Shughuli mbali mbali zinazofanywa Jeshi la
Kujenga Taifa Kambi ya Msange
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akipata Maelezo katika Banda la NHIF
Kaimu katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa Simiyu Mhe Antony Mtaka kwa Msisitizo
Na Woinde Shizza wa Globu ya jamii
Katimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa
Shaka Hamdu (MNEC) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe, Antony Mtaka
ofisini kwake Bariadi Mkoa wa Simiyu katika mazungumzo yao waligusia Nyanja
mbali mbali za kuimarisha mfumo wa kuwawezesha vijana kumudu kujiajiri ikiwa ni
kupunguza malalamiko ya kilio cha ukosefu wa ajira kwa vijana. Kaimu Katibu
Mkuu amempongeza Mkuu huyo wa Mkoa kwa
kuitikia na kutekeleza kwa vitendo agizo la Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk, John Pombe Magufuli kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda ili kutoa fursa kwa
vijana kupata ajira.
Amesifu mpango mkakati na
utekelezaji wake unaojulikana Wilaya mmoja kiwanda moja ni kampeni ambayo
imeanza kuonyesha matukio ambapo vijana wanaonekana kuanza kuchangamkia fursa
hiyo ndani ya wilaya za mkoa wa Simiyu, ametoa wito kwa wakuu wa Mikoa wengine
kuiga mfano mzuri ulioaznishwa na Mkoa wa Simiyu ili kuendana kwa pamoja na
kasi na lengo la Rais la HAPA KAZI ambapo kinadharia linahimiza maendeleo
endelevu nay a haraka katika sekta zote za kiuchumi na kijamii hususan kwa Vijana.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu amemueleza Kaimu
katibu Mkuu Shaka kuwa wamejipanga vizuri katika kubuni na kuendeleza mipango
yao sio kwa maneno bali kwa vitendo ili kuufanya mkoa huo kuwa kitovu
cha viwanda vidodogo na vya kati na viwanda vikubwa . Kwasasa Simiyu
imeanzisha kiwanda cha maziwa Wilaya ya Meatu na kiwanda cha Wilaya ya Maswa
Wakati huo Kaimu Katibu Mkuu
ametembelea na kukagua mabanda ya Maonyesho yaliyozinduliwa tarehe 7 mwezi huu
ikiwa ni miongoni mwa shuhuli za wiki ya Vijana kitaifa yaliyofanyika katika
viwanja vya Sabasaba wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu.Kaimu Katibu Mkuu
ameridhishwa na muamko wa vijana katika kuonyesha muamko wa kuitikia wito wa
Serikali wa kuwekeza katika miradi yao ya kijamii ili kumudu kujiari na
kupunguza kilio cha ukosefu wa ajira sambamba na kuwanusuru wasijiingize katika
matendo maovu.