Balozi
wa India Nchini, Sandeep Arya (kushoto) akibadilishana mawazo na Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) mara baada ya
kuwasili ofisini kwake. Lengo la ziara ya balozi huyo lilikuwa ni
kuelezea nia ya serikali ya India katika uwekezaji kwenye sekta ya gesi
nchini.
Balozi
wa India Nchini, Sandeep Arya (kushoto) akisaini kitabu cha wageni.
Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Balozi
wa India Nchini, Sandeep Arya akielezea uzoefu wa nchi ya India kwenye
uwekezaji wa uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongoza kikao na
Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya pamoja na watendaji kutoka Wizara
ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Shirika la
Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za
Nishati na Maji Nchini(EWURA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za
Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).
Sehemu
ya watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia maelezo
yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (hayupo pichani)
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa katika
picha ya pamoja na Balozi wa India Nchini, Sandeep Arya (kushoto).