MKUU WA MKOA WA MWANZA ATAKA MAHAKAMA KUREJESHA IMANI KWA WANANCHI.


Watendaji wa Mahakama nchini wamehimizwa kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu, ili kurejesha imani kwa wananchi juu ya chombo hicho muhimu katika utoaji wa maamuzi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, alitoa kauli hiyo jana kwenye Mkutano wa robo mwaka wa Chama cha Majaji na Mahakimu JMAT, tawi la Mwanza na Geita uliofanyika Jijini Mwanza.

Mongella alisema watendaji wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanapaswa kutenda haki katika shughuli zao na kuhakikisha mchango wa mahakama katika utoaji wa haki unaonekana kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu tawi la Mwanza, Francis Kishenyi, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ukerewe, alisema miongoni mwa malengo ya chama hicho ni kuhakikisha watumishi wa mahakama wakiwemo Majaji na Mahakimu wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya mahakama.


Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umejadili masuala mbalimbali ikiwemo maadili ya viongozi wa Umma katika kuwatumikia wananchi.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia