Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker
akimkabidhi Godliver Mwendo cheti cha mfanyakazi bora wa benki hiyo
katika uzinduzi a wiki ya huduma kwa mteja tawi la Msasani Jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker(katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tawi la NMB Msasani
katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa mteja leo Jijini Dar es salaam.
Meneja
wa kanda ya Kinondoni Vicky Bishubo akielezea namna benki ya NMB
imeweza kuwafikia wananchi na wateja wao kwa uharaka na madhumini yao ya
kuendelea kutoa huduma bora katika Wiki ya Huduma kwa wateja
iliyozindulia leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker
akizungumza na wateja waliofika asubuhi katika tawi la NMB Msasani na
kuwaelezea malengo yao ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akiwa na sambamba na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzane Kaganda katika kuchukua chakula.
Wateja wa benki ya NMB wakiwa wanachukua chakula.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker
akiwa anasalimia na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP
Suzane Kaganda leo katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja leo NMB
Msasani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker wakizungumza jambo na Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzane Kaganda katika
uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker
akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tawi la NMB Msasani
katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa mteja leo Jijini Dar es salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI
ya NMB, imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani kwa kuahidi
muendelezo wa huduma bora kwa wateja na kupokea ushauri kutoka kwa
wateja na wadau, huku ikisisitiza utayari katika kuelekea Tanzania ya
Viwanda.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo uliofanyika NMB Tawi la Msasani, Mkurugenzi
Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, amesema licha ya kuwa huduma bora ni
kipaumbele cha kila siku, lakini wataitumia wiki hii kuboresha zaidi,
ikiwamo kufanyia kazi maoni ya wateja.
Ineke
amesema kwamba, kutokana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano,
chini ya Rais John Magufuli, ya kuigeuza Tanzania kuwa ya viwanda, benki
yake iko tayari kuendana na kasi ya mchakato huo, ambao unategemea sana
ubora huduma za kibenki.
Ineke
ameongeza , benki yake imekuwa kinara nchini sio tu katika utoaji wa
huduma bora kwa wateja, bali pia huduma bora za kijamii kwa ujumla,
ambako imekuwa ikichangia katika sekta zote, zikiwemo za afya na elimu.
Aidha,
katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, NMB imepanga
kufanya ziara katika Kituo cha Kulelea Wazee kilichopo Kigamboni jijini
Dar es Salaam, ambako pamoja na mambo mengine, watatoa msaada na
kuhudumu kwa wazee waliopo kambi hiyo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia