Ticker

6/recent/ticker-posts

MIFUKO YA JAMII YATAKIWA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA VIWANDA ILI KUPUNGUZA TATIZO LA AJIRA HAPA NCHINI ,AWAONYA PIA WADAIWA SUGU NSSF

Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na Wadau wa mkutano mkuu wa sita wa NSSF  Wakiimba wimbo wa Taifa kabla ufunguzi rasmi wa mkutano huo jijini Arusha

Waziri mkuu Kassim Majaliwa akihutubia mkutano mkuu wa sita wa wadau wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF)unaondelea kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC jijini Arusha

Waziri Ofisi ya waziri mkuu Sera Kazi Ajira Vijana na Walemavu Jenista Mhagama Akihutubia kabla ya kumkaribisha waziri mkuu Kassim Majaliwa kuongea na wadau wa mkutano mkuu wa sita wa Nssf leo jijini Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwakaribisha wageni wanaohudhuri mkutano huo kabla haujahutubiwa na waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo jijini Arusha

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Prof.Samwel Wangwe akimkaribisha Waziri ofisi ya waziri mkuu Kazi ajira vina na walemavu Jenista Mhagama ili aweze kumkaribisha waziri mkuu kuongea na hadhara ya wadau wa mkutano wa sita wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Leo Jijini Arusha

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akitoa maelezo juu ya mfuko huo wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunngano wa Tanzania , Kasim Majaliwa na Wadau wengine wa Mfuko huo Jijini Arusha

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akipokea Tani 45 za Saruji sawa na mifuko 900 yenye thamani ya milion 15 kwa niaba ya waathirika wa tetemeko la Ardhi Kagera leo jijini Arusha alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye mkutano wa Sita wa wadau wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF

Baadhi ya Wawakilishi wa makampuni kumi ambayo yamefanya vizuri katika kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mfuko wa NSSF wakipokea zawadi zao kutoka kwa Waziri Mkuu , Kasim Majaliwa, ambapo benki ya Exim iliibuka mshindi wa Jumla, mshindi wa pili alikuwa ni Kampuni ya Bakhresa na watatu ni Vodacom Tanzania.

Waziri mwenye dhamana Kazi Ajira Vijana na Walemavu Jenista Mhagama akipokea Tunzo kwa niaba ya kampuni inayotokea mkoani Ruvuma kutoka kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa ikiwa ni mojawapo ya makampuni 10 yaliofanya vizuri katika kuwasilisha michango mikubwa kwenye mfuko wa NSSF Jijini Arusha

Baadhi ya Wawakilishi wa makampuni kumi ambayo yamefanya vizuri katika kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mfuko wa NSSF wakipokea zawadi zao kutoka kwa Waziri Mkuu , Kasim Majaliwa, ambapo benki ya Exim iliibuka mshindi wa Jumla, mshindi wa pili alikuwa ni Kampuni ya Bakhresa na watatu ni Vodacom Tanzania.

Baadhi ya Wawakilishi wa makampuni kumi ambayo yamefanya vizuri katika kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye mfuko wa NSSF wakipokea zawadi zao kutoka kwa Waziri Mkuu , Kasim Majaliwa, ambapo benki ya Exim iliibuka mshindi wa Jumla, mshindi wa pili alikuwa ni Kampuni ya Bakhresa na watatu ni Vodacom Tanzania.

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Maendeleo ya Jamii Aeishi Hillary akielezea maasuala mbali mbali ambayo kamati yake imekwuwa ikifanya katika kuendeleza sekta ya hifadhi ya jamii nchini mbele ya Waziri Mkuu leo jijini Arusha

Mkurugenzi wa Mfuko wa hifadhi ya jamii wa LAPF  Eliud Sanga, akitoa neno la shukurani baadaya ya waziri mkuu kufungua mkutano wa sita wa wadau wa NSSF  jijii Arusha.

Waziri Mkuu akiagana na Mkurugenzi wa mfuko wa pensheni wa PPF Bw William Erio, baada ya kufungua mkutano wa sita wa wadau wa NSSF leo jijini Arusha

Juu  Waziri mkuu Kassi Majaliwa akiongoza viongozi na wajumbe wa bodi kuingia kwenye ukumbi wa simba Hall kufungua mkutano wa wadau Nssf leo jijini Arusha

Waziri Mkuu akiwasili Na Kusalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa mfuko wa hifadhi za jamii NSSF Prof.Samwel Wangwe Nje ya ukumbi wa mkutano Kabla hajaufungua mkutano huo Jijini Arusha

 Na Woinde Shizza,Arusha

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) limejipanga kufanya mageuzi makubwa ya uwekezaji katika sekta ya viwanda utakaoinua viwango vya ajira na kuboresha maisha ya wanachama.

Mikakati hiyo imelenga kuitikia wito wa Rais Dk. John Magufuli wa kuijenga Tanzania kuwa nchi ya viwanda kama suluhisho la kuwakwamua Watanzania kwa kuongeza ajira.
Hayo yalielezwa  kwenye mkutano wa sita wa wadau wa NSSF uliofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).
Akifungua mkutano huo mjini hapa jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alisema Serikali inataka kuleta maendeleo kwa kuhakikisha unakuwapo  uchumi wa kati wenye kujengwa na viwanda.
Waziri Mkuu alisema anafarijika kuona NSSF ikiwa imedhamiria kwenda na mwelekeo huo kwa kupanua wigo wa uwekezaji na kuelekea katika viwanda hatua itakayoongeza ajira na kukuza uzalishaji nchini.
“Uamuzi huu utawawezesha NSSF na mifuko mingine kupata wanachama wapya na kukusanya michango zaidi na kuiwekeza   kutimiza lengo la msingi la hifadhi ya jamii.
“Nimefurahishwa na uamuzi wa NSSF na PPF kuungana kukabiliana na tatizo la sukari nchini kwa kuamua kujenga kiwanda cha sukari eneo la Mkulazi mkoani Morogoro kitakachotoa  tani 200,000 kwa mwaka.
“Lakini, pia kiwanda hicho kitatoa ajira zaidi ya 100,000 kwa Watanzania na hivyo kuongeza wanachama katika mifuko hiyo. Huu ni moyo wa uzalendo unaofaa kuigwa na kila mtu, taasisi na kampuni mbalimbali,” alisema na kuongeza:
“Kazi ya kujenga uchumi wa viwanda inaweza kufanywa kwa namna mbili, kwanza ni kwa kuvifufua vilivyopo na pili ni kwa kuanzisha viwanda vipya na kwa NSSF wao wameweza kutekeleza yote mawili.
“Mbali na ujenzi wa kiwanda hicho cha sukari, NSSF pia imeanza kazi ya uwekezaji wa kutoa mikopo kwa viwanda nchini kwa dhamira hiyo hiyo ya kuijenga Tanzania yenye viwanda.
“Nimeelezwa hapa kwamba NSSF imetoa mkopo wa Sh bilioni 3.1 za kukuza uzalishaji wa viuatilifu katika kiwanda kilichopo Kibaha, lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji.
“Natoa rai kwa taasisi zilizonufaika au zitakazonufaika na mikopo hii kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na pia kurejesha kwa wakati kwa mujibu wa mikataba   wengine nao wanufaike,”
Kuhusu suala la baadhi ya waajiri kutolipa michango kwa wakati na kusababisha usumbufu kwa wanachama, Majaliwa alisema suala hilo halikubaliki hivyo aliwataka waajiri wote nchini kuheshimu sheria na kuwasilisha michango hiyo kwa wakati.
Kwa waajiri wanaodaiwa na NSSF, alimuagiza mkurugenzi mkuu kuwaandikia barua za kutaka wawasilishe fedha wanazodaiwa mara moja na wale ambao hawatalipa ndani ya muda watakaopangiwa, wafikishwe mahakamani.
Katika mkutano huo, Waziri Mkuu aliwajulisha wadau wa NSSF kuwa Serikali imelipa Sh bilioni 722.7 kati ya madeni ya michango ya Sh bilioni 964.2.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Professa Godius Kahyarara, alisema NSSF imejipanga kuona viwanda vya ndani vikizalisha bidhaa za matumizi ya ndani na kuziuza katika soko la nje kupata fedha za kigeni.

Post a Comment

0 Comments