Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Halima Ally (28) mkazi wa kijiji cha
Moya mayoka amelalamikia kubakwa na askari wa wanyama pori Hifadhi ya ziwa
Manyara na kumtaka Rais Joseph Pombe Magufuli aingilie kati kutokana na
suala lake kufumbiwa macho na mamlaka husika.
Akizungumza kwa uchungu kuhusiana na tukio hilo Halima amesema kuwa tangu
apate mkasa huo tarehe 5/10/2011 majiraya saa kumi na mbili jioni eneo la
kitongoji cha Mayoka “C” alipokwenda shambani kuokota kuni ndipo
alipokutana na dhahama hiyo.
Aidha amesema kuwa wakati akiendelea na zoezi la kuokota kuni katika Eneo
la shamba hilo linalomilikiwa na kijiji chenye usajili *No AR kij.29*ndipo
Bi Halima alipokamatwa na askari wa wanyama pori aliyefahamika kwa jina
moja Mwasomola akidaiwa kuingia katika Eneo la hifadhi.
Aliendelea kusema kuwa askari huyo kabla ya kumbaka alimtishia kwa bunduki
yake aliyokuwa amebeba hali iliyopelekea Bi Halima kuogopa na kukaa kimya
huku akihisi maumivu kutokana na hali ya ujauzito aliyokuwa nao kutokana na
askari huyo kuendelea kutekeleza azma yake hiyo ya ubakaji.
Ameongeza kuwa baada ya kitendo hicho alikwenda moja kwa moja kumweleza
mume wake aliyefahamika kwa jina la Samweli Bura ambaye aliambatana na
mkewe huyo hadi kituo cha Poisi Magugu ambapo ilifunguliwa kesi ya
kubaka yenye jalada namba MGG/RB/1673/2011 ambapo Polisi walikwenda
kumkamata mtuhumiwa .
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa alpelekwa kupimwa afya yake na
kugundulika kuwa hajaathirika na maambukizi ya ukimwi , hivyo katika hatua
hiyo Mkuu wa kituo cha Polisi Magugu enzi hizo Thomasi Njuki ambaye
kwa sasa ni marehemu , baada ya kuuwawa kwa kupigwa risasi na
majambazi wilayani Mkuranga alipokuwa anaongoza operesheni ya kupambana
na majambazi alimshawishi mlalamikaji amsamehe mshitakiwa kwa kuwa kesi
hiyo ingemfunga ambapo mlalamikaji alimsamehe mshitakiwa
‘’Vitendo hivi vya unyanyasaji toka nilipopata mkasa wa kubakwa vimekuwa
vikiendelea hadi sasa hivyo tunaiomba serekali kupitia Raisi Magufuli
atusaidie tuweze kupata haki zetu’’ Alisema Bi Halima .
Mwathirika mwingine aliyefahamika kwa jina la Ngasso Iddi (70) naye
alilalamikia unyanyasaji huo kwa kukamatwa na kupigwa na askari
wanyama pori huku akilazimishwa kuvua suruali kisha kuchapwa viboko
na kulazimishwa kuchimba kaburi kwa vidole bila kujua kosa lake huku
akidaiwa amechunga eneo la hifadhi ambapo mifugo yake aina ya mbuzi
wapatao kumi na (11) walikamatwa na Askari wa Hifadhi hiyo huku
akitozwa faini
ya silingi elfu sitini iliyotjibitishwa na receipt No. 21079 ilitolewa
tarehe 21/06/2016.
Kufuatia mfululizo wa matukio hayo ya unyanyasaji baadhi ya wakazi
ambao pia walipata matatizo ya kubomolewa nyumba zao na
kunyang’anywa maeneo yao akiwemo Samwel Bura ambaye alikuwa
miongoni mwa wakazi wanaoishi katika eneo hilo lenye kaya nane mayoka
‘’C alisema kuwa ameathirika kwakuwa amebomolewa nyumba yake na
kulazmishwa kuondoka kwenye maeneo hayo ambayo yanadaiwa ni mali ya mamlaka
ya Hifadhi ya Taifa ambapo amepata hasara ya hekari sita za mahindi, ulezi
na mbaazi zenye jumla ya zaidi ya thamani ya shilingi million kumi.
Mbali ya athari hizo waathirika hao wamedai wameshambuliwa mara kwa mara
na wanyama pori licha ya mkazi mmoja aliyefahamika kwa jina la Agustino
Masai kuuwawa miaka ya nyuma na mbogo huku mazao ya wananchi aina ya
mahindi, maharage, ulezi na mbaazi yakiendelea kuharibiwa vibaya na
wanyama kutoka katika hifadhi hiyo pasipo mamlaka ya hifadhi kulipa fidia
waathirika.
Waathirika hao ambao wamedai kuchoshwa na manyanyaso wanayofanyiwa na
mamlaka ya Hifadhi wameamua kupaza kilio chao kwa Rais Magufuli kupitia
vyombo vya habari ili waweze kupata haki yao kwa kuwa viongozi wa eneo hilo
wameshindwa kuwasaidia licha ya kuwasilishiwa malalamiko yao pindi
wanapopata athari katika mazao yao.
Mwenyekiti wa kijiji cha Moya Mayoka John Joseph ambaye pia ni Diwani wa
kata ya Magara Wilaya ya Babati amesikitishwa na ubabe wanaofanya TANAPA
kwakunyanyasa wakazi waishio katika kijiji hicho chenye ekari elfu tisa
mia nane na arobaini, na jumla ya wakazi elfu mbili na mia nane, wakati
maeneo ya mashamba hayo yanamilikiwa kihalali na kijiji hicho.
Hata hivyo wakazi wa maeneo hayo wamekuwa na mashaka kwa risiti wanazopewa
baada ya mifugo yao kutozwa tozo kwa madai ya kuingia hifadhini wakidai
kwamba risiti hizo hazina namba ya mlipa kodi huku zingine zikiwa na muhuri
nyingine hazina huku akitoa mfano mwananchi Juma Swalehe aliyetozwa tozo ya
shilingi elfu hamsini na tano tarehe 12/6/2016 na kupewa risiti namba
21079 risiti hiyo imegongwa muhuri lakini haina namba ya mlipa kodi na
risiti namba 21082 ya tarehe 21/6/2016 Mwananchi Ngao Iddi alilipa shilingi
elfu sitini na kupewa risiti hiyo ambayo haina namba ya mlipa kodi wala
muhuri.
Afisa wanyama pori Beatrice Ndanu alipohojiwa kuhusu taratibu za kulipa
fidia kwa waathirika wa wanyama pori wanaoharibiwa mifugo na mazao yao
alisema ikithibitika mtu ameuwawa na wanyama pori wategemezi wake
watapatiwa kifuta machozi shilingi millioni moja, na aliyepata ulemavu
atapewa Shilingi laki tano na athali nyingine ndogondogo ikithibitika
atapewa shilingi elfu ishirini na tano siyo fidia bali kifuta machozi.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara Francis J. Massawe alipohojiwa
kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa halijafika rasmi mezani kwake
ameahidi kufuatilia zaidi changamoto hizo ili kukomesha uhalifu katika
maeneo ya kijiji cha Moya Mayoka ambapo ametoa wito wananchi kutokukaa
kimya, bali watoe taarifa hata kwa siri pindi wanapobaini vitendo vya
uhalifu vinavyofanywa dhidi yao.
Afisa uhusiano wa shirika la Tanapa, Psscal Shelutete alipoulizwa kuhusu
vitendo vya unyanyasaji vinavyotekelezwa na askari wa mamlaka ya hifadhi kwa
kuwapiga watu na kuwabaka pindi wanapokuwa wakichunga na kukata kuni alisema
yeye siyo msemaji wa masuala hayo bali sheria iko wazi kwa yeyote
anayevunja
sheria akilamikiwa sheria inapaswa kuchukua mkondo wake