Nyasa Boy si jina geni miongoni mwa wasanii chipukizi kutoka Jijini Mwanza. Alianza kujulikana Jijini Mwanza mwaka mmoja uliopita baada ya kufanya kazi na Mc Darada, iliyoita Chongoroa.
Mwaka huu 2016 ameachia wimbo mpya uitwao Mapenzi Nivute aliofanya na Sajna. Wimbo huo umefungua milango mipya kwani baada ya Baraka Da Prince kuusikia, hakusita kukubali kufanya kazi na Nyasa Boy ambaye anatokea kundi la Tanzania One la Jijini Mwanza.
Bonyeza HAPA Kusikiliza ama bonyeza Play hapo chini.