KIGWANGALA:WANAWAKE WANAOFANYA NGONO BILA KINGA WANAUWEZEKANO MKUBWA WA KUPATA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangala akiwa anazungumza na waandishi wa habari wanawake kuhusu tatizo la Saratani ya shingo ya Kizazi, katika Ukumbi wa Olasiti Lodge Jijini Arusha.,aliyepo kushoto kwake ni Dkt.Mathew Kasumuni kutoka hospital ya Mountmeru iliyopo jijini Arusha.

 Waandishi wa habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa Afya Maendeleo ya jamii wazee jinsia na Watoto Hamis Kigwangala,Aliyepo kushoto kwake ni Dkt.Mwanahamis Ghembe kutoka Mountmeru Hospital
Waandishi wa habari wanawake wakifuatilia kwa karibu baadhi ya majibu ya yaliyokuwa yakijibiwa na madaktari walioendesha mafunzo,mafunzo hayo yalikwenda sambaba na upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi.

Na Woinde Shizza Arusha
 

Naibu waziri wa Afya Hamisi Kigwangala amesema kuwa wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa bila kinga wapo hatarini kupata virusi vinavyoitwa HPV vinavyosababisha   Saratani ya mlango wa kizazi
 
Kigwangala amesema wanawake wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kupata saratani ya mlango wa kizazi, ambapo husababishwa kwa kufanya ngono bila kinga,huambukizwa  kwa kujaamiana .

Kigwangala amesema  kuwa kati ya wanawake 100,000 wanawake 50.9% wanaweza kupata saratani ya Shingo ya kizazi,na kati ya hao asilimia 37.5% wanapoteza maisha hivyo serikali imeanza kutekeleza utafiti wa mradi ambao utahusisha wasichana wenye umri kati ya miaka 9-14 katika wilaya ya Moshi na utakapokamilika wataanza utoaji wa chanjo hiyo kwa nchi nzima,amewataka kutokufanya ngono mapema.

Amesema kuwa Saratani ya mlango wa kizazi haionyeshi dalili wala maumivu yeyote amesema mgonjwa anaweza akawa nao kuanzia miaka 10-15 bila kujitambua huku dalili zikiwa zinakwenda taratibu sana.

Kwa upande wake Dkt.Mathew Kasumuni kutoka hospital ya mount Meru amesema kuwa dalili za Sratani ya Mlango kizazi ni kutokwa na damu bila mpangilio,kutokwa na majimaji yenye harufu kali,amewataka wanawake watakapoziona dalili hizo wawahi hospitali mapema kabla tatizo halijawa kubwa.

Aidha Masumuni amesema kuwa unaweza kujikinga ili usipate saratani ya mlango wa kizazi kwa kupima saratani ya mlango wa kizazi mapema,kupunguza idadi ya kuzaa watoto wengi,kupunguza idadi ya wpenzi wengi,ukifanya ngono watumie kinga.

Sambamba na hayo Dkt.Mwanahamisi Lyinga amesema kuwa zipo njia kuu tatu za kupima saratani ya mlango wa kizazi mabazo ni pamoja na kutumia Darubini,Upimaji wa( DNA)wa kirusi,pamoja na Via utambuzi wa kuona kwa kutumia Siki.

Kwa upande wake Sr.Noela Lyinga ambaye ni muuguzi katika hospitali ya Mountmeru ametoa elimu kwa wanawake wawe wanajikagua matiti yao kila wanapomaliza mzunguko wao wa hedhi kila mara ili kuona kama yapo mabadiliko katika matiti yao ambayo yanaweza kuleta saratani ya matiti.

Lyinga amewataka wanawake mara wanapoona dalili yeyote  ambayo siyo ya kawaida katika matiti yao wasisite wawahi hospitali mapema wakafanyiwe uchunguzi na vipimo ili kama utagundulika ugonjwa waweze kupatiwa matibabu kwa haraka zaidi. .

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia