RAIS SAMIA AWASILI MKOANI ARUSHA KUSHIRIKI MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA EAC

 



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa Machi 06, 2026 amewasili Mkoani Arusha, tayari kwa kushiriki Mkutano wa Marais wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mkutano utakaofanyika Jumamosi Machi 07, 2026 Jijini Arusha.



Kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Rais Samia amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu pamoja na Viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wa Serikali.


Mkutano wa Wakuu wa nchi za EAC utajumuisha Marais wa nchi nane zenye kuunda Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikiwa ni Mkutano wa kawaida wa 25 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine, Jumuiya hiyo itampata Mwenyekiti mpya pamoja na Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya hiyo.







About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia