BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 150 KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027.


 

 Baraza la Madiwani jiji la Halmashauri ya Jiji la Arusha limepitisha Bajeti ya jumla ya shilingi bilioni 150 kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuendelea kuboresha huduma za maendeleo kwa wananchi wa Jiji hilo. 



Bajeti hiyo imepitishwa mapema hii leo tarehe 05 Machi 2026 katika kikao cha Baraza la Madiwani, ambapo kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 60.4 kinatarajiwa kukusanywa kupitia mapato ya ndani ya Jiji. Katika bajeti hiyo, zaidi ya shilingi bilioni saba zimetengwa kwa ajili ya mipango ya mipangomiji na uboreshaji wa miundombinu ya barabara za ndani ya Jiji ili kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi kwa Wananchi.


 Aidha, kiasi cha shilingi bilioni nne kimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara za vumbi pamoja na ujenzi na uboreshaji wa mitaro ya maji ya mvua ili kupunguza changamoto ya mafuriko katika baadhi ya maeneo ya Jiji hilo. Kwa upande wa miundombinu ya barabara za ndani, jumla ya kilomita 1.9 za barabara zinatarajiwa kujengwa na kuboreshwa, sambamba na uwekaji wa kamera za usalama (CCTV) barabarani ili kuongeza ulinzi na usalama kwa wananchi wa Jiji hilo.


 Vilevile, baraza hilo limepanga kuboresha jumla ya masoko 10 ndani ya Jiji la Arusha kwa lengo la kuwapatia wafanyabiashara mazingira bora ya kufanyia biashara na kuongeza mapato ya halmashauri. Hatua hiyo inaelezwa kuwa sehemu ya mkakati wa kuimarisha maendeleo ya miundombinu na huduma za kijamii kwa Wananchi wa Arusha.



About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia