ARUSHA INA MIRADI 54 YA MAENDELEO, WANANCHI CHANGAMKIENI FURSA:MAKONDA


Katika alfa ya futari ya “Daraja la Nuru” iliyofanyika Jijini Arusha, Mbunge wa Arusha Mjini na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda amesema jiji hilo linaendelea kutekeleza jumla ya miradi 54 ya maendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Amesema miradi hiyo inalenga kuboresha huduma kwa wananchi pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo tofauti ya jiji.


Akieleza baadhi ya miradi hiyo, Makonda amesema inaendelea ujenzi wa kumbi za mikutano katika Jiji na viwanja vya michezo, Jengo ya utawala pamoja na soko la kisasa litakorosaidia kuboresha mazingira ya biashara kwa wananchi. Amesisitiza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo ni sehemu ya jitihada za serikali kuimarisha miundombinu ya kijamii na kukuza maendeleo ya Arusha.


Aidha, amewahimiza wananchi wa Arusha kuchangamkia fursa zinazotokana na miradi hiyo kwa kutumia taaluma, ujuzi na vipaji walivyonavyo. Amesema ushiriki wa makampuni ya ndani pamoja na wataalamu wa eneo hilo ni muhimu katika kujenga uchumi wa jiji na kuhakikisha maendeleo yanawanufaisha wananchi wa Arusha moja kwa moja.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia