Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa AICC kuhusiana maandalizi ya uzinduzi wa filamu maarufu ya Royal Tour inayotarajiwa kufunguliwa rasmi kesho na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu ambapo alisema maandalizi yote yamekamilika
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa maandalizi ya uzinduzi wa filamu ya Royal Tour inayozinduliwa kesho jijini Arusha na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa tanzania Samia Suluhu Hasan yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 90.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu maandalizi ya filamu hiyo Mongela amesema kuwa Hadi kufikia Leo maandalizi yameshakamilika na wanatarajia kuwa na wageni waalikwa zaidi ya elfu tano.
Amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hasan anatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege Kia kesho saa moja asubui ambapo atapokelewa na viongozi mbali mbali.
Mongela ameongeza kuwa kupitia juhudi za Rasi Samia Suluhu Hasan Kama tour guide namba moja katika utengenezaji wa filamu hiyo itandelea kuongeza chachu na mwitikio mkubwa kwa wageni watakaotembelea nchi ya Tanzania.
Amefafanua kuwa tangu kuanza kurekodiwa filamu hiyo wameona dalili za ongezeko la watalii na anaamini baada ya uzinduzi huo idadi kubwa zaidi ya wageni watafurika kutembelea vivutio vya nchi.
Mongela ametoa Rai kwa wananchi haswa wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kujitokeza nkwa wingi katika maeneo ya barabarani kwa ajili ya kumpokea Rasi na ujumbe wake kuelekea uzinduzi wa filamu hiyo.
Akiongelea hali ya usalama kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Justin Masejo alisema kuwa hali ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Arusha ipo shwari na amewatoa wasiwasi Wananchi kutokuwa na wasiwasi wa kuongezeka Kwa ulinzi kwakuwa kukiwa na matukio makubwa kama tukio hilo lazima hali ya ulinzi lazima uimarishwe.
Aidha aliwahasa kuendelea kuimarisha ulinzi kwanimpaka Sasa wanashiriana na mikoa kadhaa ili kuhakikisha ulinzi unaendelea kuimarisha.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia