Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Andrew Massawe na Mtendaji Mkuu wa Tanzania Horticulture Association(TAHA), Dkt. Jacqueline Mkindi, jana tarahe 22 April, 2022 katika ofisi ya Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma, wametia saini Makubaliano ya Ushirikiano katika kuendeleza sekta ndogo ya Kilimo cha matunda na mbogamboga(Horticulture) nchini.
Mambo yaliyowekewa msisitizo katika makubaliano hayo kati ya wizara ya Kilimo na TAHA ni pamoja na;
- [ ] Kukuza mazingira wezeshi ya ufanyaji wa biashara
- [ ] Kubadilishana teknolojia ili kukuza tija katika uzalishaji
- [ ] Utafiti na uendelezaji wa sekta ya Horticulture
- [ ] Upatikana ji wa masoko ya mazao ya Horticulture
- [ ] Kuendeleza na kuvutia sekta binafsi
- [ ] Upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati
Pamoja na mambo mbalimbali yanayohusu sekta kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi na wadau wa sekta.
Tags
HABARI MATUKIO