NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi amekabidhi Tende katika misikiti yote iliyopo katika jimbo hilo ikiwa ni kuwaunga mkono waumini wa Dini ya Kiislam.
Zoezi hilo lililosimamiwa na viongozi wa Bakwata wilaya ya Moshi chini ya Mwenyekiti wa Bakwata Hussein Jamal ambapo liliratibiwa na Ofisi ya Mbunge.
Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa BAKWATA Wilaya ya Moshi Vijijini, Jamal amemshukuru Mbunge kwa kutambua umuhimu wa kuwafuturisha waumini wa kiislamu haswa kwa tende kwani kwa kufanya hivyo ni thawabu kwa Mwenyezi Mungu.
Nao viongozi wa dini kwa nyakati tofauti wamemshukuru Mbunge kwa kuendelea kuwakumbuka katika kipindi hiki Cha mfungo wa Ramadhan.
"Kwa niaba ya waumini wote wa Kiislam tunapenda kumshukuru Mbunge kwa kuona haja ya kufanya haya, nasi kama viongozi tumefarijika sana na hiki alichokifanya. Tunazidi kumuombea kwa mwenyezi Mungu Afya tele na maisha marefu."
Zoezi hilo la kukabidhi futari kwa Jimbo la Moshi Vijijini lilihitimishwa katika Msikiti wa Mpirani uliopo katika kata ya Mabogini.
Katibu wa Mbunge alikabidhi zaidi ya
Kilo 400 za TENDE katika misikitii yote ya Moshi Vijijini