Na Fredy Mgunda,Iringa.
Naibu meya wa manispaa ya
Iringa Kenyetta Likotiko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali ya
mashindano ya E4M social centre siku ya kesho tarehe 27/03/2022 katika kiwanja
cha kimata kilichopo mtaa wa Kibwabwa kata ya kitwiru Manispaa ya Iringa kwa
mchezo kati ya timu ya Kibwabwa Fc na timu ya Dabalidali Fc ambazo zote
zinatoka katika kata ya Kitwiru.
Akizungumza na blog hiii
mdhamini wa mashindano hayo, Ibrahim Alex Manager E4M Sports Club alisema kuwa
lengo la mashindano hayo ni kutafuta wachezaji ambao wataunda timu moja kwa
ajili ya kuanza kucheza ligi ya TFF ngazi ya wilaya hadi kupanda ligi kuu hapo
baadae.
Alex alisema kuwa wamekuwa
wakijihusisha na maswala ya michezo hivyo hivi sasa wamejipanga kuhakikisha
wanaibua vipaji vipya ambavyo vitaisaidia timu ambayo wanatarajia kuinda mara
baada ya kumaliza mashindano hayo.
Alisema kuwa mashindano hayo
yamekuwa na msisimuko mkubwa kwa wananchi na wadau wa michezo katika kata ya
Kitwiru kwa kuwa ilishilikisha timu zote kutoka kata hiyo kwa lengo kwa
kuangalia namna gani kata hiyo imebalikiwa kuwa na mipaji vya wachezaji wa
mpira wa miguu.
Alex alisema kuwa jumla ya timu
nane ndizo ambazo zilishirki mashindano hayo ambazo ni
Kibwabwa,Dabalidabali,Mseke,Amani Center,Mnazi,Jamaica,Kitwiru na Juventus
ambazo zote hizo ziligawanywa katika makundi mawili ya mashindano.
Aliongeza kwa kusema kuwa
mshindi kwanza wa mashindano hayo
anajinyakulia seti moja ya Jezi pamoja na mpira moja,mshindi wa pili
atajinyakulia seti moja ya Jezi,mfungaji bora,kocha bora,goli kipa bora hao
wote watajinyakulia kiasi cha shilingi elfu hamsini kila mmoja(50000) wakati
mchezaji bora atapata kiasi cha shilingi elfu thelethini(30000).
Alex aliongeza kuwa timu yenye
nidhamu itapata kreti la soda wakati mashindano yalipokuwa yanaendelea kwenye
kila mchezo mchezaji bora alikuwa anapewa kiasi cha shilingi elfu tano(5000)
hiyo yote ilikuwa kwa lengo la kuongeza morali ya wachezaji.
Alimalizia kwa kusema kuwa
anawakaribisha wadau,wapenzi na wananachi wote katika fainali hiyo na baada ya
fainali zawadi na sherehe zote zitafanyika katika ukumbi E4M Social Centre njia
panda ya tosa maganga. Usafiri utakuwepo wa kuwachukua wachezaji wa timu zote 8
zilizoshiriki mashindano. Kikosi bora cha wachezaji 25 kitatajwa