BREAKING NEWS

Thursday, March 31, 2022

WANAWAKE WENGI WANAKABILIWA NA TATIZO LA UELEWA WA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII


 Mkurugenzi wa taasisi ya Zaina foundation ya Jijini dar es salaam Zaituni Njovu  akiongea na  waandishi wa habari wakati walipokuwa wakitoa mafunzo ya siku mbili  ya usalama mtandaoni kwa wanahabari  wanawake wa mkoa wa Arusha lengo likiwa kuwawezesha kufanya majukumu yao kwa ufanisi zaidi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya Gran melia iliopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha





waandishi wa habari  na Mkurugenzi wa Zaina foundation Zaituni Njovu  wa tatu kulia  wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya ufunguzi  mafunzo ya siku mbili  ya usalama mtandaoni kwa wanahabari  wanawake wa mkoa wa Arusha lengo likiwa kuwawezesha kufanya majukumu yao kwa ufanisi zaidi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hotel ya Gran melia iliopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha




Imebainika kuwa bado jamii hususa ni ya wanawake wanakabiliwa na tatizo la uelewa hasa Kwa matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.


Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa taasisi ya Zaina foundation ya Jijini dar es salaam Zaituni Njovu wakati akiongea na waandishi wa habari wakati walipokuwa wakitoa mafunzo ya siku mbili ya usalama mtandaoni kwa wanahabari wa mkoa wa Arusha lengo likiwa kuwawezesha kufanya majuku yao kwa ufanisi zaidi.



Alisema kumeonekana kuwa wanawake wengi wamekuwa hawana uelewa mpana kuhusiana na matumizi sahihi ya mitandao hii ,hawajatambua umuhimu sahihi ya hii mitandao hii ya kijamii,ni namna gani watumie mitandao hii kwa usahihi zaidi katika mawasiliano ambayo yana tija katika maisha yao.


"Sisi kama zainafoundation tuliona kwamba kwa wanawake kuna upungufu mkubwa wa kuelewa umuhimu wa mtandao hawajui matumizi sahihi ya mitandao katika kazi zao ikiwemo katika biashara zao ,elimu ,uchumi biashara na mawasiliano yenye tija katika biashara zao wanawake wengi yale mauthui ambayo wanayatuma katika mitandao yao ya kijamii bado ubora wake upo chini ukilinganisha na makundi mengine "



Alisema wanawake wengi wamekuwa wanapeleka mauthui ya fanifani ambayo baadae yanakuja kuwatafisiri vibaya ,muda mungine yana wahukumu , na hata kufikia sehemu ya kukuta wanawake wapo katika swala la ukatili wa kijinsia mtandaoni.


Alisema mpaka sasa zaina foundation imeshafikia mikoa nusu ya Tanzania nzima ikiwemo mikoa ya Dar es salaam ambapo ndio makao makuu yao yapo,Arusha,Tanga ,mtwara na mikoa mingine ila wanampango wa kuendelea kutoa elimu ya usalama mtandaoni Kwa wanawake wa nchi nzima


Akiongea mara baada ya kupata mafunzo hayo mmoja wawana habari wanawake aliejitambulisha kwa jina la Grace Macha alisema kuwa mafunzo haya yatawasaidia kufahamu usalama wa vifaa vyao vya kazi pamoja na kujua ni wakati gani sahihi wa kuweza kuweka habari mitandaoni na kuchambua habari ambazo hazifai kuweka katika mitandao ya kijamii 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates