BREAKING NEWS

Tuesday, March 29, 2022

MREMA NA MKE WAKE KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII NCHINI




 Mrema akiwa na mke wake


Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Mrema Machi 28, 2022 amemtambulisha rasmi Mkewe Doreen Kimbi katika ukumbi wa Keys hoteli uliopo Moshi. 


Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema amesema yeye na mke wake Doreen Kimbi wanatarajia kwenda fungate katika vivutio vya utalii nchini ikiwa ni moja ya jitihada zake za kuunga mkono mipango ya Serikali ya kukuza utalii wa ndani.


Moshi. Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labour Part (TLP) Agustino Mrema amesema yeye na mke wake Doreen Kimbi wanatarajia kwenda fungate katika vivutio vya utalii nchini ikiwa ni moja ya jitihada zake za kuunga mkono mipango ya Serikali ya kukuza utalii wa ndani.


Mrema na mkewe Doreen Kimbi walifunga ndoa Marchi 24, 2022 katika kanisa katoliki parokia ya Uwomboni jimbo katoliki la Moshi, tukio ambalo lilivuta hisia za watu wengi na leo amemtambulisha rasmi mkewe huyo.


Akizungumza na vyombo vya habari leo jumatatu machi 28, 2022 mjini Moshi Mrema amesema amepokea salamu mbalimbali za pongezi ikiwemo kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.


Mrema amesema Doreen kwa sasa ni mke wake na kwamba watafanya kazi ya kizalendo ya kukuza utalii kwa kwenda kufanya fungate katika vivutio vya utalii nchini ambapo watatembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tarangire, Manyara na Ngorongoro.


Amesema tayari amezungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii na kumuahidi ushirikiano nae ili kufanikisha ziara yao ya kutembelea vivutio vya utalii nchini hatua ambayo wanaamini itachochea na kukuza utalii wa ndani.


Amesema ziara hiyo ya kutembelea vivutio vya utalii wameipa jina la 'Mr&Mrs Mrema Honeymoon tour’ na kwamba itaanza aprili 9, mwaka huu na lengo ni kumuunga mkono Rais Samia na kazi anazofanya za kukuza utalii wa ndani

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates