Na Woinde Shizza , ARUSHA
Waandishi wa habari wametakiwa watumie kalamu zao kuisemea vyema nchi yao pamoja na serikali Kwa ujumla huku Ili kuendelea kuilinda amani ya nchi
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Philbert Luhunga alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wa mikoa ya Arusha , Kilimanjaro na Manyara katika mafunzo ya siku nne yaliolenga kuwajengea uwezo wa kuandika habari za tafiti mbalimbali zinazotolewa na wanasayansi na kuzifikisha kwa wananchi kwa lugha rahisi yaliyoandaliwa na tume hiyo Kwa uthamini wa serikali .
Alisema kuwa katika kufanya kazi zao ni vyema waandishi wa habari wajiheshimu ,wajitambue pamoja na kufanya kazi Kwa weledi wa hali ya juu huku wakiweka mbele maslahi ya nchi yao.
Alisema kuwa lengo la kuandaa mafunzo hayo Kwa wanahabari ni kuwaelimisha zaidi na kuwajengea uwezo mzuri wa kuandika habari za tafiti mbalimbali zinazofanywa na wanasayansi wetu na kuzifikisha Kwa Wananchi Kwa lugha rahisi ambayo itamuwezesha mwananchi wa kawaida kuielewa vyema.
"watafiti wamekuwa wanafanya tafiti mbalimbali baada ya hapo wanaandika taarifa za tafiti walizofanya kwa lugha ambazo si rafiki jambo ambalo wanapopelekewa taarifa hizo wanashidwa kuzifanyia kazi wengine hawaelewi kutoka ana lugha ambazo watafiti hao wamekuwa wanazitumia hivyo ndio maana tumewaita nyie mjifunze Ili tafiti hizi mkizipata muandike kwa lugha nyepesi ambayo itamuwezesha mwananchi kuelewa"alisema
Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt Baraka Msangi alisema kuwa tafiti hiI zikiandikwa kwa lugha rahisi na zikawafikia wananchi itawasaidia kufanya maamuzi katika kutatua yao ya kila siku
Aidha aliwataka watafi hao kuandika machapisho yao kwa ufupi ili kuweza kumrahisishia mwananchi kusoma na kuelewa kiuraisi
. ikiwemo dawa za kutibu magonjwa ya wanawake ,dawa za kutibu magonjwa ya ngozi ,dawa za kutibu magonjwa ya macho pamoja na dawa ya ugonjwa wa uzio.