afisa kutoka Taasisi ya Lions Clubs International Tanzania kanda ya tanzania 411 c, Masonya Kabwena wa kwanza kushoto ,kulia ni mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Arusha (FFU) Mekidadi Galilima katikati ni afisa mazingira kutoka taasisi ya Lions Clubs International Tanzania Evah Benson wakipanda miti kwa pamoja akipanda mti katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Arusha (FFU) wakati taasisi hiyo ilipopeleka jumla ya miti 300 kwa ajili ya kupanda katika mazingira yanayozunguka kikosi hicho ,afisa huyo alisema wanampango wa kupanda miti elfu 10000 katika mkoa wa Arusha
Ili kuweza kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi
wananchi wametakiwa kujijengea tabia ya
kupanda miti angala mmoja katika kipindi cha msimu wa mvua ili
kuweza kubadilisha Tanzania yetu pamoja na kukabiliana na tatizo la
mabadiliko ya tabia nchi
Hayo yameelezwa na afisa kutoka Taasisi ya Lions
Clubs International Tanzania kanda ya tanzania 411 c, Masonya Kabwena alipokuwa akiongea na
waandishiwa habari wakati walipokwenda kupanda miti katika kambi ya FFU Arusha ambapo alisema
lengo la kuja kupanda miti ni pamoja na kuhamasisha utunzaji wa mazingira
Alisema kuwa taaasi yao imejipanga kupanda jumla ya miti zaidi
ya laki moja kwa nchi nzima ya katika
kipindi cha mwaka mmoja lengo likiwa ni
kutunza mazingira ,kupata matunda kutengeneza makazi ya viumbe vingine kama wadudu na ndege pamoja na kupendezesha nchi
yetu
Alisema kuwa katika kuanza kupanda miti wameanza na kupanda
miti 300 katika kambi ya FFU Arusha
ambapo baada ya hapo wataenda kupanda
miti mingine katika kambi ya FFU NJiro pamoja na taasisi nyingine na kwa mkoa
wa Arusha wanampango wa kupanda jumla ya
miti elfu 10000.
Kwa upande wake afisa mazingira kutoka taasisi ya Lions Clubs International Tanzania Evah Benson alisema kuwa wanampango wa kupanda
miti elfu 10000 katika mkoa wa Arusha na
wataotesha katika taaasisi mbalimbali
zikiwemo mashule ,hospitali na katika sehemu za wazi , huku akibainisha kuwa
mbali na hivyo kupanda miti pia wanawahimiza wananchi kupanda miti kwani miti
ni uhai na pia miti inafanya Tanzania inakuwa ya kijani
Akiongea mara baada ya kupokea na kupanda miti hiyo mkuu wa kikosi cha
kutuliza ghasia mkoa wa Arusha (FFU)
Mekidadi Galilima aliishukuru taasisi
hiyo kwakutoa miti hiyo na kubainisha
kuwa wataitunza na kuhakikisha miti hiyo inakuwa na kufika pale ambapo imekusudiwa kwani tunapotunza mazingira na nyenyewe
yanatutunza
Alisema kuwa wanashukuru kwa namna ambayo wamewatia nguvu na
kuwawezesha wameweza kupata miti ambayo itakuwa ni faidi kubwa kwao na hata kwa
kizazi kijacho ambapo pia aliwahakikishia
kwa sababu taasisi yao ni nyeti na kubwa wanaouwezo mkubwa kuhakikisha kwamba miti hiyo
wataitunza kama vile walivyowaamini na
kuwaletea maana hata katika masomo yao wanayofundishwa wanavyokuwa katika masomo
yao wamekuwa wakifundishwa maswala ya
kutunza mazingira .