BREAKING NEWS

Saturday, March 26, 2022

NAPE NNAUYE AJIVUNIA MAFANIKIO YA WIZARA YA HABARI MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI




Na Hamida Ramadhan Dodoma



WAZIRI wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema Katika kipindi Cha Mwaka mmoja na Kipindi kifupi cha Wizara hiyo mpya wanajivunia mafanikio makubwa kwa miradi inayotekelezwa na kusimimiwa na wafanyakazi wa Wizara ya Habari.



Ameyasema hayo leo Machi 25 2022 jijini hapa wakati akifungua kikao Cha Baraza la wafanyakazi kikao kilicholenga kujadili mwenendo wa utekekezaji wa bajeti ya wizara kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 na Mpango wa bajeti ya wizara wa Mwaka wa fedha 2022/ 2023 na zoezi linaloendelea la Mfumo wa Anwani za makazi .



Amesema Miradi miwili mikubwa wanayoifanya ni pamoja na ujenzi wa mkongo wa Taifa na wa pili kujenga Mfumo wa anwani za makazi ambapo amesema Miradi hiyo ni muhimu kuwepo na bila miradi hiyo sekta zingine zitashindwa kufanya kazi



" Kwa mujibu wa Ilani ya chama cha mapinduzi CCM tulitakiwa kujenga Mfumo wa anwani za makazi kwa muda wa miaka 5 lakini imekuwa tofauti na hivyo Sasa tunajenga Mfumo kwa muda wa miezi 5 ,"



Na kuongeza Kusema " Watu wamekuwa wakijiuliza maswali tutawezaje kutekeleza Mradi huo kwa Kipindi kifupi hivyo tukumbuke kuwa Jambo hilo litawezekana Kama tutakuwa wamoja kwani tumefika mahali pazuri ambapo tathimini inaonyesha tumefikia asilimia 30 mpaka 40 na tarehe 22 mwezi wa tano mwaka huu tunakabidhi bila kushindwa," amesema.



Aidha amesema Tunapokuwa tunakabidhi Mfumo huu lazima tutambue lazima mchango wa kila mmoja uonekane katika kuhakikisha Mfumo huu unafanikiwa kwani jambo hilo sio dogo litabaki kwenye historia ya Vizazi ,"amesema Nnauye



Akizungumzia Siku 360 za Rais Samia Suluhu Hassan amesema wameweza kuanzishwa Mradi Mkubwa wa Tanzania ya kidigitali na wote wafanyakazi waliopewa dhamana kubwa watahakikisha Tanzania ya kidigitali inawezekana.



Pia ametoa wito kwa Menejimenti kuhakikisha Wizara inakuwa na mazingira mazuri ya utendaji kazi pamoja na mafanikio haya lazima tuendelee kupigania mazingira mazuri ya wafanyakazi mahusiano mazuri baina ya utendaji kazi wafanyakazi na kuhakikisha Haki na stahili za wafanyakazi zinatolewa kwa wakati



Hata hivyo amewataka watumishi wa wizara hiyo kuhakikisha wanatenda haki bila kujali Mkubwa au mdogo huku akisisitiza kuwa wizara haiwezi kustawi bila ya kuwepo kwa upendo,haki na kuheshimiana.



Nnauye amesema, kwa kuzingatia uhusiano baina ya haki na Wajibu katika kutekeleza majukumu waliojipangia ni Wajibu kufahamu na kusimamia kwa ufanisi utekekezaji wa sera Mpango mkakati sheria Kanuni na miongozo taratibu mbalimbali zinayohusu haki Wajibu na stahili za wafanyakazi pamoja na Utawala bora.





"Mimi ni muumini wa haki hivyo niwaombe watumishi wote katika ngazi mbalimbali mjitahidi katika kutenda haki na Kama ukiona kwenye moyo wako haki inakusumbua kuitekeleza basi wizara hii haikufahi japo tunataka tusimamie haki," amesema.



Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi amesema kikao hicho ni kikao Cha Siku mbili na watapitia mwenendo wa bajeti ya Mwaka wa fedha 2021/2022 na pia Mwaka wa fedha 2022/23.



Pia amesema katika kikao hicho watajadiliana suala la anuani za makazi kwani suala hilo ni jukumu kubwa kwa kuhakikisha wanafanya jambo hilo kikamilifu.




Kwa Upande wake Katibu wa Baraza la wafanyakazi tawi la Habari na Mawasiliano TUGHE Leah Sanga amesema kwa Upande wa Tughe hawana malalamiko Wala hoja iliyowasilishwa hiyo ni ishala nzuri inayoonyesha utulivu na amani utawala,nakuomba wafanyakazi wote wa wizara kushirikiana Ili kuleta tija kazini.



Mwisho

 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates