BREAKING NEWS

Sunday, March 13, 2022

WATAKIWA KUNYWA MAZIWA ANGALAU BILAURI MOJA KWA SIKU


 Na Woinde Shizza , ARUSHA


Watanzania wametakiwa kujenga itikadi ya kunywa maziwa maziwa Kwa wingi kwani yana virutubisho vyote tofauti na bidhaa zingine.

Hayo yamebainishwa na meneja uzalishaji wa Kiwanda cha Grande Demam kilichopo wilayani Meru mkoani Arusha wa Jacline Kinabo wakati akiongea na waandishi wa habari katika maonyesho ya kimataifa ya kilimo (TanzFood) yanayofanyila katika viwanja vya magereza vilivyopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha mkoani hapa .

Alibainisha kuwa watanzania wengi wamekuwa hawana desturi ya kunywa maziwa mara Kwa mara huku wengine wakiwa hawajui faida za kunywa maziwa hivyo ni vyema wakachunguza faida za zake na kuanza kutumia.



Alisema maziwa hufanya mambo mengi mazuri kwa ajili ya afya ya binadamu am, ni wazi kuwa, vitamini na virutubisho vilivyoko katika maziwa ni muhimu kwa ajili ya ngozi bora. Ni vyema kunywa angalau bilauri moja ya maziwa kila siku.

Alisema faida nyingine kuimarisha men ambapo alisema
Maziwa ni chanzo bora cha madini ya kalisiamu, hivyo basi maziwa ndicho kitu halisi kinachohitajiwa na meno yetu. Pia maziwa huzuia kutoboka na kuoza kwa meno. Kalisiamu hufyonzwa na miili yetu kukiwa na vitamini D; hivyo jitahidi kunywa maziwa kwani maziwa huwa na vitamini D hukuakibainisha faida nyingine kuimarisha mifupa

"Ni ukweli usiopingika kuwa watoto wanahitaji kunywa maziwa ili kuimarisha ukuaji wao,pia ni kweli pia watu wazima wanahitaji kunywa maziwa ili kulinda na kuimarisha mifupa yao dhidi ya magonjwa kama vile udhaifu wa mifupa (osteoporosis),Maradhi haya huzuiliwa kwa kalisiamu ipatikanayo kwenye maziwa na ambayo hufyonzwa kutokana na uwepo wa vitamini D"

Alisema maziwa yana mchango mkubwa katika ukuaji wa misuli,hili ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa, Wanariadha wengi hunywa maziwa baada ya mazoezi, hii ni kwa ajili ya kuupa mwili virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kujijenga tena ,pia huzuia maumivu ya misuli pamoja na kurudisha ute ulipotea kwenye misuli wakati wa kazi mbalimbali aidha pia husaidia kupunguza uzito
Utafiti unaonesha kuwa wanawake wanaokunywa maziwa hupunguza uzito zaidi kuliko wale wasiokunywa,Inashuriwa kunywa maziwa wakati wa chakula cha jioni au unapokula matunda pia maziwa yanaweza kutumiwa kama kileta hamu ya kula yaani appetizer.

Alisema pia huondoa msongo wa mawazo
Hebu fikiri juu ya vitamini na virutubisho vilivyoko kwenye maziw hivi huweza kuondoa msongo baada ya kazi nyingi za siku, inashauriwa kunywa angalau bilauri (glass) moja ya maziwa ya uvuguvugu. Hili litakusaidia kukuondolea msongo katika misuli na neva zako za fahamu pia uzuia maumivu wakati wa hedhi
Wanawake wengi wanakabiliwa na maumivu wakati wa hedhi Maziwa yamedhibitishwa kuzuia na kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa.



Aidha pia alisema maziwa hupambana na maradhi mengine
Kwa miongo kadhaa tafiti zimebaini kuwa maziwa huzuia magongwa kadha wa kadha kama vile shinikizo la damu na kiharusi, Inaaminika pia maziwa hupunguza sehemu (cholesterol) mwilini na kuongeza uwezo wa macho kuona,pia  alisema baadhi ya watafiti wameeleza kuwa unywaji wa maziwa huzuia ania fulani za saratani.

Alibainisha kuwa kutokana na faida hizo ndio maana kampuni yao imeamua kutoa elimu ya unywaji maziwa Kwa Wananchi pamoja na kuwaelimisha namna ya kuhifadhi maziwa pamoja na jinsi ya kusindika maziwa hayo katika hali ya usafi  

Aliwasihii Wananchi kutumia maziwa yao kwani yanatengenezwa katika hali ya usafi pia wanayachemsha Kwa utaalamu ambao unafanya maziwa hayo kubaki na vitamini zote zilizopo katika maziwa. 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates