Aidha Baraza hilo limeishauri serikali kuanza kuwatambua wazee hao na kuwalipa pensheni kama wenzao wa Zanzibar wanaolipwa na serikali yao jambo litakalosaidia kuwapunguzia makali ya maisha .
Akiongea katika uzinduzi wa baraza hilo la wazee katika Kata ya Moshono Jijini hapa, mwenyekiti wa baraza hilo Mkoa wa Arusha, Mhina Sazua,alisema yapo matukio mengi yanayowafanya wazee wapoteze maisha kabla ya muda wao ikiwemo kukosa uangalizi suala ambalo amesema ni wakati mwafaka Kwa serikali kuwapa uangalizi kwani wazee ni hazina ya Taifa.
Akitolea mfano ukanda wa kaskazini kumekuwepo na matukio ya wazee kukuta wamefungiwa kwenye vyumba vidogo na wakati mwingine kulazwa na Mbuzi na kupatiwa chakula kupitia dirisha dogo baada ya kufanywa ndondocha (Zezeta) Kwa lengo la kuvuta Mali kishirikina suala ambalo linaondoa thamani ya wazee
"Ninao ushahidi vijana wa Siku hizi wanatafuta utajiri kupitia miili ya wazazi wao baada ya kudanganywa na waganga wa kienyeji kuwa ukimua baba yako au kumfanya ndondocha utapata Mali nyingi na kujenga nyumba nzuri na kumiliki Mali nyingi "alisema Mwenyekiti
Sazua aliongeza kuwa licha ya serikali kuwawekea mazingira mzuri ya kupata uduma ya matibabu Bure kupitia bima ya Afya lakini huduma hiyo haipati badala yake wananyanyasika na kukosa matibabu Kwa sababu ya hawalupi chochote.
Awali risala ya baraza hilo la wazee iliyosomwa na katibu wa wazee, Emanuel Ndelimana wazee hao walilalamikia huduma ya bima ya Afya kufuatia kadi zao kumalizika Muda wake na kusababisha usumbufu wa kukosa huduma ya Afya kwenye vituo vya Afya.
Wazee hao wameiomba serikali kuweka utaratibu wa kuwalipa pensheni wazee wote hapa nchini ili wapate fedha za kujikimu kwani baadhi ya wazee hali zao ni mbaya Sana baada ya kutelekezwa na Jamii zao
Kwa upande wake diwani wa Kata ya Moshono , Miriam Kisawike, aliwaahidi wazee hao kwamba atashughulikia baadhi ya changamoto kinazowakabili likiwemo suala la bima ya Afya kwa kulifikisha kwa mkurugenzi wa jiji la Arusha Kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
"Wazee wangu niwaombe Kwa dhati ya Moyo wangu suala la bima ya Afya nitalishughulikia ipasavyo na wale ambao kadi zao zimeisha Muda wake watoe taarifa Kwangu au kwa mtendaji wa Kata na kero zingine nitazipeleka kunakohusika likiwemo suala la Tasaf"alisema