BREAKING NEWS

Wednesday, March 23, 2022

WANANCHI WATAKIWA KUENDELEA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI

 



Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (AUWSA) Mhandisi Charles Kondela katikati akikata keki Kwa ajili yakuwalisha wateja wao katika kilele Cha week ya maji kimkoa kilichofanyika katika viwanja vya makao makuu ya ofisi hiyo jana kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya week ya maji mkoa wa Arusha ambaye pia ni mkuu wa idara ya ufundi na usafi wa mazingira kutoka Mamlaka ya maji safi na maji taka muhandisi Upendo Shushu
Mtoa elimu wa Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Arusha (AUWSA )Gemma Ibrahimu akitoa elimu kwa wateja waliouthuria katika mabanda ya  maonyesho ya wiki ya maji yaliokua yakifanyika katika viwanja vya ofisi ya AUWSA vilivyopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha mkoani Arusha maonyesho yaliofikia kilele 


Na Woinde Shizza , ARUSHA


Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (AUWSA) Mhandisi Charles Kondela amewataka wananchi kuendelea kutunza mazingira ili kulinda vyanzo vya maji.


Aidha pia amewataka wananchi kufichua wale wote ambao wanatumia maji isivyo halali pamoja na wale ambao wanaiba maji kwani wanavyofanya hivyo wanaipa serikali hasara

Aliyaeleza hayo wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Maji yaliyofikia tamati jana kwenye Viwanja vya makao makuu ya AUWSA Mhandisi Kondela alisema mazingira yanatakiwa yalindwe katika nyanja zote kuanzia kwenye vyanzo vya maji, miradi inayojengwa na kupata ushauri kutoka Baraza la Mazingira NEMC na Wizara husika.

Amesema, katika sheria ya mazingira ya 2004 imeweka wazi kuwa kwenye kila mradi uandaliwe tathimini itakayoangalia athari za kijamii na kibinadamu.



Alisema, upandaji wa miti unapunguza mmomonyoko wa ardhi na kusaidia ardhi kushika na shughuli za kijamii zinazofanyika pembezoni za Mto husababisha udongo kuingia na kiwango cha tope kuwa kingi na kupelekea kina cha mto kupungua na kusababisha mafuriko ,ambapo pia aliwataka wananchi watunze mazingira ili yawatunze 

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya week ya maji mkoa wa Arusha ambaye pia ni mkuu wa idara ya ufundi na usafi wa mazingira kutoka Mamlaka ya maji safi na maji taka(AUWSA) muhandisi Upendo Shushu alisema kuwa wamejipanga kuwapa Wananchi huduma bora zaidi 

Alisema lengo la kufanya maathimisho haya kimkoa ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali walizokuwa wanazifanya ,ambapo pia alitaja kauli mbiu ya maathimisho hayo inasema maji chini ya aridhi azina isiyooneka Kwa maendeleo endelevu.

Alisema kuwa kwa upande wawateja wale sugu wamewaita kulingana na kauli yao mbiu yao ya mteja wetu fahari yetu wamewaita katika week hii ya maji Ili waweze kuingia nao mkataba wa kulipia kidogo kama asilimia 25 afu ingine watalipia polepole huku wakiendelea kupata maji safi na salama

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates