
Mgeni Rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kitaifa ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha akiwa katika banda la Mtandao wa Jinsia Tanzania ( TGNP). Kushoto ni Mkurugenzi wa TGNP, Bi. Lilian Liundi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella na viongozi mbalimbali wakipokea maandamano ya wanawake kutoka makundi mbalimbali kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kitaifa ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela ameitaka jamii kupambania usawa wa kijinsia na ulinzi wa watoto kwa kizazi cha usawa na haki ili kufikia maendelo ya haraka.
Aidha kauli mbiu hii inalenga kuhamasisha uwajibikaji kwa wote kuleta usawa wa kijinsia pamoja na kukumbushana umuhimu wa usawa katika kuchochea ukuaji wa kiuchumi na maendeleo jumuishi.
Ambapo amewataka kujitokeza kuhesabiwa kwa maendeleo ya kumkomboa mwanamke na taifa kuwa na kizazi cha usawa wa kijinsia nchini.
Mongela ameyasema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliofanyika kimkoa katika uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Awali Mkuu wa mkoa wa Arusha alizindua kanzidata ya Taifa ya wanawake na jinsia iliyoandaliwa na Mtandao wa kutetea masuala Kijinsia nchini TGNP kwa kushirikiana na wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu.
"Kinamama wakienda mbele katika maendeleo yataigusa jamii kubwa kwa maendeleo makubwa ngazi ya familia kwa kuleta mapinduzi makubwa ya kuleta usawa katika mapambano ya usawa wa kijinsia"
Kwa mujibu wa Asilimia 3 rasilimali hupotea kwa ajili ya athari za ukatili wa kijinsia hii inaelekea tukitaka kupunguza umaskini tumuwezeshe mwanawake kiuchumi katika kuimarisha na kuleta maendeleo ya kasi.
Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Amon Mpanju amesema kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu jitokeze kuhesabiwa,imelenga kumuwezesha mwanamke kiuchumi
Alisema kuwa haki na usawa nchini inatekeleza uwezeshaji wanawake kiuchumi kuhakikisha tunawezesha kila moja kuwa na usawa wa kiuchumi kijamii kiutamaduni na sekta zote.
Mary Oneal Balozi wa Ireland nchini alieleza kwamba Juhudi ni nyingi za serikali ila siku hii msingi ni kutafakari na kujiuliza tulipo tunapoelekea katika kumkomboa mwanamke kiuchumi duniani
"Lengo kuu ni kumuewezesha mwanamke kiuchumi kijamii na kiutamaduni kufikia usawa na haki katika kuwezesha wanawake kiuchumi kuwa na mipango hatamuzi inayolenga kizazi cha usawa kuleta mustakabali wa ustawi wa jamii ili kunufaisha watu wa jinsia zote kwa usawa"
Alisema kwamba sasa ni muda wa kutambua na kuthamini nafasi ya mwanamke katika kuchochea ukuaji wa kiuchumi na maendeleo jumuishi kutupa fursa ya kutathmini utekelezaji wa maazimio na mikataba ya kimataifa kikanda na kitaifa yenye lengo la kuimarisha jitihada za kuleta amani, ambapo Tanzania imepiga hatua duniani katika kuleta usawa wa kijinsia
Mwanamke akiendesha mtambo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kitaifa ambayo yanafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha