mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Mhandisi Profesa Fredrick Kahimba akiongea na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya mafunzo ya kuandika habari za sayansi na teknnolojia yalioandaliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (COSTECH)
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Taasisi ya Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) imetekeleza Azimio la nchi kutokuwa tegemezi kwa kutegemea nchi nyingine kwa kuhakikisha kuwa Tanzania inajitegemea kiviwanda kwa kutengeneza teknolojia mbalimbali zinazosaidia kupunguza utegemezi.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Mhandisi Profesa Fredrick Kahimba wakati akiongea na waandishi wa habari walipokuwa katika ziara ya mafunzo ya kuandika habari za sayansi na teknnolojia yalioandaliwa na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (COSTECH) yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Arusha na kufuatiwa na ziara ya siku mbili ya kutembelea taasisi zinazojishulisha na kazi za sayansi na teknolojia ambapo moja ya taasisi waliotembelea ni hiyo
Alisema kuwa wameijenga hiyo dhana na kusaidia kupunguza utegemezi wa uagizaji wa bidhaa nje ya nchi bidhaa ambazo zinaweza kutengenezewa na watanzania wenyewe hivyo wameweza kubuni na kutengeneza vifaa tiba hivyo kwani kwa muda mrefu serikali imekuwa ikiagiza vifaa hivyo kutoka nje ya nchi.
“Kwa mfano katika sekta ya Afya serikali ilikuwa inaagiza vifaa tiba nje kwa asilimia 90 na vinavyotengenezwa hapa nchini ni asilimia 10, sisi TEMDO tuliliona hilo na sasa tunatengeneza vifaa tiba ili kuhakikisha kwamba tunapunguza matumizi mengi ya fedha za kigeni zisizo na sababu kwa kuagiza vifaa tiba na kuhakikisha Sasa vifaa hivyo vinatengenezwa hapa nchini kwa bei nafuu na vinawafikia walengwa kwa wakati,”Alisema Mhandisi Profesa Kahimba.
Alisema kuwa vituo vya afya vilivyojengwa nchi nzima kwa sasa vina uhakika wa kupata vifaa tiba vyake mkutoka katika taasisi hiyo ya TEMDO badala ya kuagiza tena kutoka nje ya nchi
“Tuna teknolojia ya sekta ya kilimo, afya kama nilivyoeleza awali, sekta ya uvuvi, na zaidi sekta ya viwanda vikubwa na vidogopia tunatengeneza mashine mbalimbali ikiwemo ya kukamulia Alizeti na nifafanue tu mashine hii ya kukamulia mafuta ya Alizeti tumepewa fedha na Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu (COSTECH)ambapo tumekabidhiwa kiasi cha shilingi millioni 128 kati ya hizo milioni 65 ni kwaajili ya kutengenezea mashine hii ya kukamulia mafuta ghafi ya alizeti na fedha zinazobaki tunatekelezea miradi mingine”Alifafanua.
hii ndio mashine ambayo Tume ya Taifa ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu
(COSTECH)imetoa fedha kwa ajili ya kuibuni ambapo kiasi cha shilingi
milioni 65 kimetumika kwaajili ya kutengenezea mashine
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia