Mwenyekiti wa Tlp Taifa na Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini Doctar Agustino Mrema ametangaza kufunga pingu za maisha na mkewe mpya Siku ya Alhamisi katika parokia ya uwomboni kijijini kwake kiraracha Mkoani Kilimanjaro Mrema anafunga ndoa hiyo mara baada ya kumpoteza mke wake Mwaka Jana Rose Mrema kwa kufariki Dunia .
Akiongea na A24Tv Mrema amesema amepata Binti mwenye umri Mdogo mweupe ambaye ni chaguo lake na watafunga pingu za maisha Mara baada ya kufuata taratibu zote za kikanisa pamoja na ulipaji wa mahari .
Amesema kilicho msukuma kuoa ni kumpata Msaidizi wa kumsaidia katika maisha yake kwani yeye ni Mzee na anaitaji mtu wa karibu wa kumwangalia na kumsaidia kwa ukaribu
Mrema amesema anashukuru familia yake kwa kumkubalia kumpata mke .