BREAKING NEWS

Monday, March 21, 2022

MTOTO WA FARU JOHN AFARIKI DUNIA

   



Faru Rajabu mtoto wa aliyekuwa Faru maarufu Tanzania Faru John, amefariki dunia jumapili usiku katika hifadhi ya taifa ya serengeti akiwa na miaka 43.


Shirika la hifadhi za taifa Tanzania TANAPA limetangaza kifo cha Faru huyo aliyepata umaarufu kupitia kwa baba yake Faru John aliyefariki mwaka 2015 akiwa na miaka 47.


Kamishna msaidizi mwandamizi wa mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete amesema kuwa Faru Rajabu amefariki kutokana na uzee na ameacha watoto, wajukuu na vitukuu kadhaa.


"Kama ilivyokawaida ya kanuni za asili za uhifadhi huona namna bora ya kuhifadhi mwili wa Faru Rajabu" alisema Shelutete.


Faru Rajabu alizaliwa Ngorongoro mwaka 1979 na mwaka 1993 alihamia katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


Aliwahi kupongezwa na Hayati Rais John Magufuli kwa kufanikiwa kuongeza idadi kubwa ya faru kwenye uzao wake katika eneo la ikolojia ya Serengeti na hata kufikia hatua ya kupelekwa katika hifadhi nyingine ili kuongeza faru.


Wastani wa maisha ya Faru weusi ambao wapo katika kundi la wanyama walio katika hatari ya kutoweka hukadiriwa kuwa kati ya miaka 35 hadi 40.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates